ASKARI MAGEREZA AFUNGWA KWA KUJITONGOZESHA KWA WAFUNGWA...
https://roztoday.blogspot.com/2012/06/askari-magereza-afungwa-kwa.html
Mwanamke Ofisa Magereza ambaye amekiri kuwaandikia badua za kimapenzi na kuwapigia simu wafungwa wanne amehukumiwa kifungo cha miezi 12 jela wiki hii.
Zanib Khan mwenye miaka 27, alitumia zaidi ya masaa kumi kuongea na wahusika wa dawa za kulevya na wakabaji.
Mfungwa mmoja kati ya hao alisema hawezi kusahau "alipokuwa akikatiza kwenye mageti na kumwona mwanamke wake mrembo".
Mwingine amenukuliwa akimbusu 'midomo yake na mwili' na kuzungumzia jinsi alivyotaka kumona miguu midogo ya bibi jela angani wakati wakifanya mapenzi.
Barua hizo, zilizagaa kutoka eneo lake la kazi Gereza Kuu la Brixton, na kisha baadaye zikakutwa kitandani kwake nyumbani kwa wazazi wake.
Baada ya kukamatwa kwake ilifahamika hapo kabla aliwahi kuadhibiwa kwa kushinda kuweka wazi kwamba baba yake mzazi alikuwa akitumikia kifungo cha miaka minne jela kwa makosa ya uhamiaji, na kwamba rafiki yake wa kiume alikuwa jela kwa uporaji.
Japokuwa Zanib amekiri kuwasiliana na wafungwa wanne, polisi wanahisi amekuwa akishirikiana kwa karibu na wafungwa watatu kati yao.
Jopo lililokuwa likimtetea Zanib limesisitiza kwamba licha ya kwamba barua hizo zilihusisha 'mambo ya kimapenzi', zote zilikuwa za kufurahisha.
Mwendesha Mashitaka Robin Du Preez alisema, kati ya Machi na novemba 2011: "Zanib aliendeleza mahusiano yasiyokubalika na wafungwa wanaotumikia kifungo kwenye Upande A wa gereza la Gereza Kuu la Brixton.
"Walikuwa Timothy Iyegbe, Daryl Smith na Jason Graham. Alikuwa anawajibika kwao gerezani na hakuweka bayana chochote kuhusu mahusiano yao, kwa mujibu wa Sheria za Gereza."
Smith na Iyegbe wote walikuwa wakihusika na dawa za kulevya.
Preez, alichambua mashitaka yaliyopita ya nidhamu kuhusu Zanib, "Baba yake alikuwa akitumikia kifungo na yeye alijiunga na Magereza (Januari 2009) siku 12 baada ya baba yake kufungwa.
Pia alishindwa kuweka wazi mahusiano yake na mfungwa, Wahid Khalique."
Maisha ya mapenzi yenye utata ya Zanib yalibainika Oktoba 7, 2011, wakati simu ilipokutwa kwenye kizimba cha Jason Graham kwenye gereza la wazi la Ford. Aliwahi kufungwa Gereza Kuu la Brixton.
Preez alisema simu hiyo alikuwa akiitumia kuwasiliana na Zanib. Uchunguzi ulibaini kwamba namba hiyohiyo alitumia Zanib kuwasiliana na 'wafungwa kadhaa' wakiwamo Iyegbe na Smith.
Kati ya Machi 10 na Novemba 22, 2011, kulikuwa na masaa 10 ya maongezi ya simu kati ya Zanib na wafungwa.
Preez alifafanua kwamba wafungwa wanaruhusiwa kupiga simu kwa idadi maalumu ya namba zilizohakikiwa na kurekodiwa. Iyegbe alikuwa na namba ya Zanib ambayo aliisevu kama 'mama yake' na Smith alikuwanayo kama 'mpenzi wake'.
Polisi walipitia mazungumzo yaliyorekodiwa ya dakika tatu na nusu kati ya Iyegbe na Zanib ya Agosti 28, 2011.
Preez amesema Zanib alimalizia simu kwa kusema 'Nakupenda,' kama alivyoambiwa. Zanib alikamatwa Januari 28, 2011 baada ya nyumba yake iliyoko Ilford, East London kupekuliwa na kukutwa barua hiyo. aliacha kazi siku hiyo.
Barua kutoka kwa Wahid Khalique zilikuwa 'hazina chochote kibaya,' wakati barua kutoka kwa Smith na Iygbe zilikuwa na michoro mingi, mahakama ilielezwa.
Wakili wa Zanib, Anand Beharrylal, alisema upunguzaji makali wa mapenzi katika maneno yaliyotumika kwenye barua hiyo ilikuwa 'wa hali ya juu.'

Jaji David Higgins alimweleza Zanib, ambaye alikiri kukiuka taratibu katika ofisi ya umma: "Ulifanya kwa makusudi na kuendelea kwa hiari yako na kuendelea kwa kiasi kikubwa kuvunja uaminifu."