CHEKA TARATIBU...

Marais wawili wa Afrika Mashariki walikuwa wakisafiri kwa ndege yao ndogo ndipo ghafla Rais mmoja ambaye alikuwa rubani akaruka nje kwa kutumia Parachuti.
Huku Rais aliyebaki akiwa hajui kuendesha ndege, akaamua kuchukua redio na kuomba msaada.
"Mayday, Mayday! Rubani wangu karuka kutoka kwenye ndege kaniacha peke yangu nikiwa sijui chochote!"
Waongoza ndege kutoka chini wakamsikia na majibizano yakawa hivi:
CHINI: "Umesema Rubani?" RAIS: "Ndio, kaniacha angani, karuka kwa parachuti!" CHINI: "Usijali mheshimiwa. Nitakuongoza uweze kutua salama, we fanya kama nitakavyokwambia. Kwanza nataka unipatie 'kimo' na 'sehemu ulipo'." Kwa kujiamini Rais akajibu, "Nina zaidi ya futi sita na nimekaa mbele kabisa!" Duh, ama kweli usilolijua...

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item