BONDIA "THE CANNON" KUPOTEZA PAMBANO NJE YA ULINGO...
https://roztoday.blogspot.com/2012/06/bondia-cannon-kupoteza-pambano-nje-ya.html
Bondia Shannon "The Cannon" Briggs anaweza kupoteza moja katika rekodi yake safi ya masumbwi sababu anakabiliwa na uwezekano wa kushindwa mahakamani katika kesi ya madai ya karibu Dola za Marekani nusu milioni.
Ofisa habari wake wa zamani, Kali Bowyer amemshitaki bondia huyo akidai alimsaidia kupata Dola za Marekani milioni 2.8 mwaka 2009, lakini hakuwahi kumpa kamisheni zake.
Kali amedai kuwa anamdai Shannon Dola za Marekani 420,000 kwa huduma zake na kwa mujibu wa Mahakama ya South Carolina, bondia amekataa kupokea hati ya mashitaka.
Mahakama ilitoa hukumu ya moja kwa moja wiki hii bila mshitakiwa kuwepo ikiamuru bondia huyo kulipa deni lote mara moja.
Juhudi za kumpata Shannon zilishindikana kutokana na kutopokea simu.