MWIGIZAJI LINDSAY LOHAN APATA AJALI MBAYA YA GARI...

Mwigizaji Lindsay Lohan amepata ajali mbaya ya gari na kukimbizwa chumba cha wagonjwa wa dharura kwenye Hospitali ya Santa Monica UCLA mjini Los Angeles, imeelezwa.
Lindsay alikuwa akiendesha gari lake aina ya Porsche jeusi kwenye Barabara Kuu ya ufukwe wa Pacific mjini Santa Monica ndipo akaligonga kwa nyuma trela lenye magurudumu 18 majira ya mchana. Gari lake hilo kwa sasa halifai.
Imeelezwa Lindsay hakwenda hospitali kwa kutumia gari la wagonjwa licha ya kwamba lilifika eneo la tukio kwa kazi hiyo.
Imefahamika kwamba baada ya kuchukuliwa vipimo kadhaa, mwigizaji huyo ameruhusiwa kutoka hospitali muda mfupi baadaye.
Mwakilishi wa Lindsay ameeleza, mwigizaji huyo alikuwa akielekea kupiga picha za filamu ya "Liz & Dick" ndipo alipojibomeza gari alilokuwa akiendesha kwenye trela la lori na gari hilo kusambaratisha kabisa.
Aliongeza, "Mwigizaji huyo hakupata majeraha makubwa katika ajali hiyo. Kwa sasa yuko fiti na kwamba ameelekea kupiga picha za filamu hiyo."

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item