BONDIA PACQUIAO AWASHITAKI WAHASIBU WAKE KUHUSU KODI...

Bondia Manny Pacquiao amewashitaki wahasibu wake akiwashutumu kwa kufanya makosa mengi ya kimahesabu kuhusu masuala ya kodi katika kampuni yake.
Mashitaka hayo aliyofungua bingwa huyo wa masumbwi ni dhidi ya kampuni ya VisionQwest Resource Group. Mwaka jana kampuni hiyo ilimshitaki Manny kwa kushindwa kulipa gharama za ada yao.
Sasa Manny anasema katika hati yake ya mashitaka kwamba kwanini mtu alipi ada kwa wahasibu ambao si tu kwamba wamefanya 'makosa kadhaa' kwenye malipo ya kodi lakini 'wamekabidhi mahesabu na ushauri kuhusu kodi ulio chini ya kiwango."
Mashitaka hayo yamefunguliwa na mwanasheria Dan Petrocelli aliyeendesha kesi iliyomfunga OJ Simpson, akidai VisionQwest 'hawana utu' kwa kulenga kuvuna faida kubwa ya haraka kutoka kwa Manny.
Manny pia anawatuhumu kwa kuhodhi kumbukumbu zake za malipo ya kodi kinyume cha sheria.
Cha kufurahisha ni kwamba: Kwenye hati yake ya mashitaka Manny amejiita "Bondia bora duniani wa Pauni kwa Pauni."
Pia amedai kuwa yeye ni mwanamichezo wa sita anayelipwa zaidi duniani, akifikisha mapato ya Dola za Marekani milioni 40 kuanzia nusu ya pili ya mwaka 2008 hadi nusu ya kwanza ya mwaka 2009.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item