KIJANA AKUMBWA NA MARADHI YA AJABU...

KUSHOTO: Sain Mumtaz. KULIA: Sain akiwa pamoja na familia yake.
Kijana ambaye amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya ajabu iliyomwacha akiwa na kichwa kikubwa mno, miguu na mikono, anatafuta kwa udi na uvumba tiba itakayomwezesha hatimaye kupata upendo.
Sain Mumtaz mwenye miaka 22, ameharibika kabisa wajihi wake kufuatia maradhi hayo ya ajabu yaliyomsababishia baadhi ya sehemu zake za mwili kuendelea kukua kwa kasi.
Amekuwa akikubalika miongoni wa majirani zake kwenye mji wa Lahore, nchini Pakistan, lakini maradhi hayo yamemwingiza kwenye matatizo ya matibabu yanayoendelea na kujikuta akishindwa hata kujitokeza mitaani.
Inadhaniwa kwamba Sain anasumbuliwa na dalili za kipekee za uwiano mbovu wa Proteus kama zile zilizomuathiri 'Tembo Mtu' Joseph Merrick, kutokana na kukua kwa kasi na kuharibika sura na fuvu la kichwa chake.
Sian ambaye amekata tamaa anaamini kwamba maradhi aliyonayo ni laana aliyoshushiwa na Mungu wa Hukumu, ikimwacha awe mtu asiye na thamani na aliyevunjwa moyo.
Lakini familia yake na marafiki wamekuwa wakimpa moyo mno na sasa anaonekana kurejesha furaha ya maisha.
Majirani wamekuwa wakimtambulisha kama 'rafiki mwenye umbo kubwa' na kwamba wanaonekana kupata tiba kwa ajili ya Sian ambaye amerejesha matumaini kwamba atampata mwanamke wa maisha yake.
Alisema: "Nimekuwa katika hali hii tangu kuzaliwa kwangu. Sura yangu, mikono na miguu vyote vimepishana ukubwa na watu wanahisi siko kama binadamu wengine.
"Lakini mimi niko timamu na kuelewa kila kitu, ninaishi maisha kama mtu mwingine yeyote licha ya kwamba familia yangu akiwamo mama, baba, kaka zangu na dada zangu wote wamezaliwa bila hali hii.
Watu wamekuwa wakinikimbia. Lakini sasa wamekuwa wakinichukulia kawaida na kukaa na kuongea nami ninapotoka.
"Wananiita rafiki yao. Siku moja natumaini kupata tiba na kukutana na mwanamke ambaye atanipenda."
Sain hakuwahi kwenda hospitali kwa matibabu tangu alipokuwa kijana mdogo wakati alipoelezwa kuwa na dalili za madhari hayo na hakuna kinachoweza kufanyika kumsaidia.
Kama akifanikiwa kurekebisha maradhi hayo hakutakuwa na chochote cha kupunguza uzito wa nyayo zake zilizokithiri kwa ukubwa.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item