EVANDER AUZA JUMBA LAKINI HUENDA AKAAMBULIA PATUPU...
https://roztoday.blogspot.com/2012/06/evander-auza-jumba-lakini-huenda.html
Habari njema ni kwamba mkongwe wa masumbwi duniani, Evander Holyfield hivi karibu amefanikiwa kuuza jumba lake kwa Dola za Marekani 7,500,000!!!
Habari mbaya ni kwamba ilikuwa katika mnada wa hadhara. Evander alikopa fedha benki mara mbili ya kiasi hicho. Pia anadaiwa zaidi ya Dola za Marekani 200,000 kama marejesho ya kodi.
Kwa mujibu wa nyaraka zilizowasilishwa Georgia, jumba la Evander lenye ukubwa wa futi za mraba 54,000 kwenye eneo la ukubwa wa eka 234 lililoko nje kidogo ya Atlanta limeuzwa katika mnada wa hadhara Machi 6, mwaka huu, lakini sehemu ya fedha hizo zitakwenda moja kwa moja kwenye malipo ya kodi.
Kiasi kilichobakia, kwa mujibu wa nyaraka, Evander alikopa zaidi ya Dola za Marekani 14,000,000 kwa ajili ya jumba hilo pamoja na Dola za Marekani 2,500 za gharama ufilisi. Haijafahamika kama benki itambana kumalizia deni hilo.
Juhudi za kumpata Evander kwa njia ya simu hazikufanikiwa kutokana na simu zote zilizopigwa kukosa majibu.