MGAHAWA WAKANA KUHUSIKA NA MARADHI YA LASORDA...

Mmiliki wa mgahawa wa Kitaliano ambako Tommy Lasorda (pichani) alikula chakula siku moja kabla ya kupata shambulio la moyo amesisitiza, mgahawa wake unaofanya vema hauhusiki na matatizo yaliyomkumba gwiji huyo wa mchezo wa baseball.
Anthony Bamonte, mmiliki wa mgahawa wa Bamonte wenye miaka 112 sasa ulioko mjini Brooklyn ameeleza, shambulio la moyo lililompata Lasorda Jumatatu iliyopita 'halihusiani na chakula cha hapa. Shambulio la moyo ni Shambulio la moyo tu."
Kuhusu alichokula Lasorda Jumapili usiku, Bamonte amesema, aliagiza chakula cha kawaida na kushushia na mvinyo mwekundu. Tatizo liko wapi hapo?
Bamonte alisema hawezi kushauri chakula kingine tofauti kwa Lasorda atakapotembele mgahawa huo mara nyingine, akiongeza, "Tommy ni Tommy. Huwezi kumbadilisha Tommy."
Lasorda alikimbiza hospitali ya New York-Presbyterian Jumatatu iliyopita, ambapo madaktari walimpandikiza kifaa katikam moyo wake kuzibua mshipa mkubwa wa damu ulioziba.
Mwakilishi wa timu ya Dodgers amesema Lasorda amepumzika kwa starehe kitandani na kwamba yuko katika hali nzuri.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item