MADADA WAWILI NDUGU WAKUTWA WAMEKUFA HOTELINI...

PICHANI JUU: Hoteli ya Phi Phi walimofia madada hao wawili ndugu. PICHANI CHINI: Mashuhuda wakisaidia kubeba miili ya madada hao.
Madada wawili wa Canada wamekutwa wamekufa kwenye chumba cha hoteli walimopanga nchini Thailand.
Polisi wa Thailand wanahisi Audrey na Noemi Belanger wenye umri wa miaka 20 na 26, inawezekana kuwa walijeruhiwa na "sumu kali kwenye chakula."
Maofisa hao wamesema madada hao walikuwa kwenye matapishi, majeraha katika ngozi na walikuwa wakitokwa damu kwenye fizi zao. Kucha za vidoleni na miguuni za madada hao zilikuwa rangi ya bluu na kulikuwa na damu chini yake.
Wanafunzi hao mashuhuri wa chuo kutoka mji mdogo wa Quebec, jirani na mpaka na Maine, waligunduliwa na mhudumu wa Hoteli ya Phi Palm katika kisiwa maarufu cha watalii cha Phi Phi, Ijumaa kwa mujibu wa gazeti la Bangkok Post.
Luteni Kanali Rat Somboon wa Kituo cha Polisi cha Jimbo la Krabi, anahisi wanawake hao walikufa kati ya masaa 12 na 20 hadi pale miili yao ilipogundulika.
Miili ya madada hao itafanyiwa uchunguzi muda mfupi ujao kuthibitisha wamekufa vipi.
Polisi wanahisi sumu ya kwenye chakula na walisema uchunguzi wa mwanzo haukuonesha dalili zozote za vurugu kwenye chumba chao cha hoteli. Uchunguzi umethibitisha dosari kadhaa.
"Hakukuwa na dalili zozote za mapigano, wala unyang'anyi, lakini tumegundua aina tele za madawa yakiwamo ibuprofen, ambazo zinaweza kusababisha madhara makubwa tumboni," alisema Luteni Kanali wa Polisi Jongrak Pimthong.
Wanawake hao, kutoka familia inayofahamika sana kwenye mji wa Pohenegamook, karibu maili 150 Kaskazini-mashariki mwa Jiji la Quebec, waliingia hotelini humo Jumanne.
"Walitoka na kurejea kwenye chumba chao hotelini usiku wa siku hiyo, lakini wakakaa ndani ya chumba chao kwa siku nzima ya Jumatano," alisema Luteni Siwa Saneha wa Polisi wa Kisiwa cha Phi Phi.
"Mhudumu aligonga mlango kwa ajili ya kutaka kusafisha chumba Alhamisi, lakini hakukuwa na majibu, hivyo mhudumu akafikiri wanawake hao walikuwa wakiendelea kupumzika na kuamua kuondoka zake."
Alisema kwamba haikuwa hivyo hadi jana kwamba mfanyakazi wa hoteli alipotaka kujua usalama wao na kutumia ufunguo maalumu kuingia chumbani humo.
"Kulikuwa na matapishi mengi chumbani, na miili yote ilionesha dalili zinazofanana (ya kiwewe). Walikuwa na majeraha kwenye ngozi na walionekana wakiwa na damu kwenye fizi. Pia, kucha zao za mikononi na miguuni zilikuwa za bluu," Kanali Somboon alisema.
"Tutakuwa na wataalamu watafanya uchunguzi kwenye matapishi na sampo za mkojo uliochukuliwa eneo la tukio kujaribu kujua sababu za vifo."
Miili ya madada hao kwa sasa imehifadhiwa katika Hospitali ya Krabi mjini Krabi.
Shangazi mkubwa wa madada hao, Colette Belanger, amesema alisikia kuhusu vifo hivyo katika taarifa ya habari.
"Nilihisi kwamba walikuwa Audrey na Noemi," alisema.
Kisiwa cha Phi Phi kilichoko Bahari ya Andaman kiko umbali wa maili 500 kusini mwa Bangkok.
Katika tukio linalofanana na hili Mei, 2009, mwanamke wa Kimarekani na mwanamke wa Kinorway walikuwa baada ya kutapika sana na kuharisha kwenye nyumba ya kulala wageni huko Phi Phi. Chanzo cha kifo hakikuelezwa hadi sasa.

Post a Comment

  1. I am gеnuinely thankful to the owner of thіѕ website who haѕ
    shared thiѕ wonderful pаragraph at at thіs
    plаcе.
    Feel free to visit my web site ; brand name laptops

    ReplyDelete

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item