TAASISI YA MARY J. BLIGE YAIGEUZIA KIBAO BENKI...
https://roztoday.blogspot.com/2012/06/taasisi-ya-mary-j-blige-yaigeuzia-kibao.html
Taasisi ya Mary J. Blige imesema kuwa benki inayowashitaki ilifanya upumbavu kuwakopesha watu waliofilisika, hivyo ni makosa yao wenyewe kushindwa kulipwa, hii ni kwa mujibu wa nyaraka za kisheria.
Kama ilivyoripotiwa hapo awali, Taasisi ya Mar J. Blige and Steve Stoute Foundation for Advancement of Women Now ilishitakiwa na Benki ya TD baada ya kuichukua mkopo wa Dola za Marekani 250,000 Juni, 2011 na taasisi hiyo kuweza kulipa Dola za Marekani 400 tu hadi muda wa mwisho waliokubaliana kulipa deni hilo Desemba mwaka jana.
Sasa Taasisi hiyo imejibu mashambulizi kwenye hati ya mashitaka ikidai kama benki wangefanya kazi yao ipasavyo, wangegundua kundi hilo halikuwa na uwezo wa kurejesha na kwamba kamwe lisingekopesheka tangu awali.
Zaidi, taasisi imedai mwanamke ambaye alisaini mkopo huo hakuwa na mamlaka ya kufanya hivyo, kitu ambacho ni sababu nyingine zaidi za kuweza kunyimwa mkopo huo.
Kesi hiyo bado inaendelea.