MAMA ALIYEBAMBWA NA DAWA ZA KULEVYA ASIMULIA MKASA MZIMA...
https://roztoday.blogspot.com/2012/06/mama-aliyebambwa-na-dawa-za-kulevya_11.html
Mwezi uliopita Mama Sandiford mwenye miaka 55 alitawala vichwa vya habari pale alipolazimishwa kuketi mbele ya meza iliyokuwa na pakiti za dawa za kulevya aina ya cocaine.
Maofisa Uhamiaji wa kisiwa cha Indonesia walidai mzigo huo uliokuwa na thamani ya Pauni za Uingereza milioni 1.6, ulikutwa umebandikizwa kwa pembeni ndani ya mkoba wake.
Mama huyo alikiri kubeba kitu fulani, lakini amesisitiza hakujua nini kilichokuwamo ndani yake.
Waingereza wengine wawili, Julian Ponder mwenye miaka 43 na mpenzi wake Rachel Dougall mwenye miaka 38 ambao wanasemekana ndio vinara wa mpango huo, na Paul Beales nao pia wamekamatwa.
Wote wanne, ambao bado wanahojiwa na polisi wamedai kutokuwa na hatia.
Akiwa amevalia sare yake ya wafungwa rangi ya machungwa mwezi uliopita, Mama Sandiford alionekana kushitushwa pale alipokumbana na kamera za mapaparazi na kujaribu kuficha uso wake.
Hofu yote kwisha jana, alikuwa akikatisha kwa kilio kila baada ya dakika kadhaa huku akionesha kuchanganyikiwa wakati kwa mara ya kwanza alipoelezea jinsi maisha yake yalivyopinduka kabisa kufuatia mfululizo wa matukio yasiyo ya kawaida.
"Naweza kuhukumiwa adhabu ya kifo," alisema huku akilia, wakati akivuta mikono ya mmoja wa waandishi. "Naogopa sana. Naweza kufia hapa."
Mpaka sasa, amesema, amekuwa akifungwa kwa kamba kwenye kiti kwa siku mbili huku akielekezewa bastola kichwani mwake.
Akishikiliwa kwenye chumba cha pekee kilichojitenga, amekuwa akilala kwenye godoro jembamba mno. "Ni vigumu kama kuwa kwenye chumba chenye mvuke kwa wakati wote siku nzima."
Mahojiano yake na gazeti moja yalifanyika kwenye selo katika kituo kimoja cha polisi. Wakati akitembea kwenye varanda kukutana na waandishi alionekana kupata kigugumizi cha miguu na huku mikono yake akiwa kakunja.
Akiwa amefadhaika na wazi kuwa na kiwewe, pia alikuwa amechoka. Hii, alisema, ni kwa sababu walinzi wamekuwa wakimfanya ashinde macho kutokana na kuwasha taa kila baada ya dakika 30 kwenye kizimba chake.
Mama sandiford alisema alikubali kubeba begi kwenda nayo Bali sababu mtoto wake wa kiume, Elliot mwenye miaka 21, alikuwa akipewa vitisho na kundi la wauza dawa za kulevya.
"Nilifahamu walichokuwa wakitaka nifanye kilikuwa kitu cha hatari," alisema. "Hawakuwa wakinitaka nipeleke jibini au kitu kizuri lakini sikufahamu pia kama ilikuwa pesa, dhahabu, vito, bunduki, bangi au heroin. Sikujua chochote.
"Nilifungua begi nikahisi ubao umeweka ndani ya begi pembeni. Nikaweka vitu vyangu juu yake na kujaribu kujisahaulisha."
Majaribu yake yakaanza pale polisi walipogundua 'kiwanda cha dawa za kulevya' jirani na ghorofa ambamo Elliot alikuwa akiishi nchini Uingereza.
"Kwa sababu fulani, sikuelewa kwa nini, wenye kiwanda cha dawa za kulevya walimuhisi mwanangu kwamba amewapa taarifa polisi," amesema.
"Nilipanga ghorofa lile kwa jina langu na ghafla nikapigiwa simu na mtu niliyefahamiana naye zamani. Bila shaka nilimfahamu mtu huyu miaka 20 iliyopita wakati nikiishini mjini London.
"Alikuwa rafiki wa marafiki. Nilikuwa nikimuona maeneo hayo mara moja moja. Lakini mara nyingine alikuwa akinipigia simu na kunialika kwa kahawa. Tulikutana kwenye mgahawa wa McDonald's. Tuliongea maongezi ya kifamilia tu. alinieleza alikuwa na binti mdogo na nikamweleza nina watoto wa kiume wamekua na kwamba niliishi India.
"Nilikuwa nimerejea tu Uingereza kusaidia kumhamisha Elliot kutoka kwenye ghorofa hilo na kuchukua mwanangu mkubwa, Louis ambaye alikuwa ametoka kifungoni. Louis alikuwa akijihusisha na magenge ya wahuni na kuishia kuhukumiwa kifungo cha miaka sita na miezi minane jela kwa unyang'anyi. Nadhani hicho ndicho kitu kibaya zaidi kilichonitokea, lakini kosa langu liko wapi.
"Nilikwenda India na kurejea Uingereza Machi kubadili pasipoti yangu. Ndipo Elliot akanieleza yuko mbioni kutoroka maana amekuwa akitishiwa kuuawa. Alisema, "Mama unatakiwa kunisaidia."
"Nilipokea simu kutoka kwa mtu ambaye simfahamu akisema mwanangu ni mchongezi na wangemuua kama asingeweka mambo sawa."

Itaendelea...