MAWAZIRI WAWILI WAFA AJALI YA HELIKOPTA, CHANZO HALI MBAYA YA HEWA...


 ZILIZOTUFIKIA:  Uchunguzi wa awali umeonesha kwamba helikopta iliyoanguka na kuua mawaziri wawili na abiria wengine wanne ilisababishwa na hali mbaya ya hewa.
Helikopta mpya kabisa ya polisi iliyokuwa ikiwasafirisha Waziri wa Usalama wa Ndani wa Kenya, Profesa George Saitoti, Naibu wake Orwa Ojode, marubani wawili na walinzi wawili ilianguka na kuwaka moto dakika 10 tu baada ya kuruka kutoka Uwanja wa Ndege wa Wilson majira ya Saa 2:20 asubuhi.
Ikumbukwe kuwa, vifo vyao vimekuja wakati wa kumbukumbu ya miaka mitano tangu kufariki kwa wabunge wawili, Lorna Labosso na Kipkalya Kones ambao pia walikufa kwenye ajali ya ndege Juni 10.
Serikali ya Kenya imetangaza siku 3 za maombolezo ambapo bendera itapepea nusu mlingoti.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item