MKONGWE WA BASEBALL ALAZWA KWA MARADHI YA MOYO...
https://roztoday.blogspot.com/2012/06/mkongwe-wa-baseball-alazwa-kwa-maradhi.html
Mkongwe wa mchezo wa Baseball, Tommy Lasorda kwa sasa amelazwa hospitali ya New York baada ya kushambuliwa na maradhi ya moyo mapema wiki hii, imeelezwa.
Lasorda mwenye miaka 84 ambaye alijiuzulu kazi yake ya ukocha wa mchezo huo mwaka 1996 kabla ya kupata maradhi ya moyo, alikuwa jijini New York kuiwakilisha timu ya L.A. Dodgers katika kuandaa rasimu ya katiba ya MLB, ambayo imeanza jana.
Vyanzo vya habari vimesema, shambulio la moyo lililompata 'sio kubwa' na kwamba Tommy anatarajiwa kuwa sawa na kuna mpango wa kuruhusiwa wakati wowote kesho.
Watu kwenye kikao hicho walianza kuhisi kitu fulani hakiko sawa leo baada ya Lasorda kushindwa kuhudhuria kuwasilisha mapendekezo ya Dodgers kwenye muswada huo.
Lasorda alionekana mwenye afya njema Jumapili iliyopita, akisaini vitabu vya mashabiki wakati walipokutana na waandishi wa habari pamoja na kupata chakula kwenye mgahawa wa Kitaliano wa Brooklyn na mkongwe mwenzake Lou Piniella.