AMA KWELI USAFIRI KAFIRI...
https://roztoday.blogspot.com/2012/06/ama-kweli-usafiri-kafiri.html
Abiria wakindandia lori huku likiwa katika mwendo kasi katika kijiji cha Muze, wilaya ya Sumbawanga, lililokuwa likielekea mjini Sumbawanga juzi. Licha ya kwamba barabara hiyo inakatiza Bonde la Ziwa Rukwa ambalo ni maarufu kwa kilimo cha mpunga na ufuta, hakuna usafiri wa mabasi kwa ajili ya wanavijiji waishio kwenye maeneo hayo kuwahakikishia usalama wao kutokana na ubovu wa barabara na hivyo kulazimika kudandia malori ya mizigo.