MKONGWE WA BENDI YA FLEETWOOD MAC AJIUA KWA RISASI...
https://roztoday.blogspot.com/2012/06/mkongwe-wa-bendi-ya-fleetwood-mac-ajiua.html
Mwanamuziki wa zamani wa bendi iliyotamba kwa muziki wa rock ya Fleetwood Mac amekutwa amekufa nyumbani kwake Nashville jana baada ya kujipiga risasi, hii ni kwa mujibu wa Polisi wa Nashville.
Mwili wa Bob Welch mwenye miaka 66 ulikutwa na mkewe majira ya mchana. Kwa mujibu wa polisi, Bob alijipiga risasi mwenyewe kifuani.
Polisi wamesema Welch, ambaye alikuwa na matatizo ya kiafya hivi karibuni, ameacha ujumbe kuelezea kwamba kajiua.
Welch alikuwa mpiga gitaa na mwimbaji wa bendi ya Fletwood Mac kuanzia mwaka 1971 hadi 1974.
Alianzisha kundi la Waingereza la muziki wa rock mjini Paris mwaka 1976, na akatamba kwa vibao kadhaa vikiwamo vya "Sentimental Lady" na "Ebony Eyes."