MWANAUME AKIRI KANISANI KULA KINYESI NA MIKOJO...

https://roztoday.blogspot.com/2012/06/mwanaume-akiri-kanisani-kula-kinyesi-na.html
Nabii mwenye utata wa Nigeria, T.B. Joshua bado anagonga vichwa vya habari vya magazeti mbalimbali duniani.
Hatahivyo, safari hii si kuhusiana na usemi wa Kinabii au mgeni wa kisiasa...
Jumapili ya Aprili 15, mwaka huu, kanisa mashuhuri la Joshua mjini Lagos lilishuhudia tukio la kukera la kuigiza pale mtu mmoja alipotoa ushuhuda wa tabia mbaya ya kutia kinyaa.
Mukaika Malomo, Mnigeria aliyeishi Ujerumani kwa miaka 16, aliungama kutawaliwa na tabia ya ajabu ambapo mara kwa mara alikunywa mseto unaochefua wa zabibu, mbegu za kiume na mkojo.
Kwa mujibu wa Malomo, mhitimu wa Chuo cha Uandishi wa Habari cha London, tabia hiyo ilianza usiku mmoja akiwa kwenye chumba cha gereza huko Ujerumani. "Niliamka usiku wa manane na ibilisi akaniamuru kuamka kitandani," aliueleza umati wa waumini wa SCOAN.
"Sauti hii ngeni ilinielekeza kwenda chooni, nijisaidie haja kubwa na kuichanganya na mbegu zangu na mkojo. Nikachanganya mkojo, mbegu na kinyesi na kumeza kila kitu."
Malomo, ambaye amewahi kufanya kazi katika kampuni moja ya kuuza saladi mjini Munich kabla ugomvi uliotokana na ulevi kumsababishia kutupwa jela, alifafanua kuwa hasira za ajabu na dhamira ya kupigana ghafla vikamuandama.
"Baada ya kumeza mseto huo, nguvu ya ajabu ikanijia. Nikajihisi kama vile Mungu mdogo. Ilinizidia na nikawa mbabe na mwenye hasira kama vile kuna nguvu ya ziada kutoka dunia nyingine imeingia mwilini mwangu. Nilikuwa tayari kwa vita. Tangu hapo, kwa zaidi ya miaka 15, nimebobea kwa kula kinyesi changu, mkojo na mbegu. Siwezi kuacha."
Aliendelea simulizi ya maisha yake duni, akielezea jinsi kila alipoendekeza matakwa hayo ilivyomsababishia vurugu zaidi. "Baada ya kuachiwa kutoka jela, kila mara nilikuwa nikipigana Ujerumani. Wakati mwingine, polisi walilazimika kuzingira mtaa mzima kujaribu kunidhibiti na nilikuwa nikitumia chupa pekee. Niliendelea kuchoma bila kuchoka sababu ya nguvu hii iliyoingia ndani yangu."
Watu waliomo kanisani walidhibiti hofu zao wakati ufunuo wa Malomo ukiendelea. "Haikuwa kinyesi changu pekee; katika matukio mengi, nilienda kwenye vyoo vya mitaani hapa Nigeria na Ujerumani na kula hapo hapo."
Alielezea mseto huo kuwa ni chakula kwake. "Nilifurahia. Sikusikia harufu yoyote. Nilikula kama vile nakula 'eba' (mlo maarufu Nigeria) au kitu kingine kama hicho."
Malomo, amefunga ndoa na msichana mwenye asili za Ujerumani na Hungary ambaye wamefanikiwa kupata mtoto wa kiume aliyezaliwa wakati Malomo akiwa jela, alielezea jinsi alivyotunza siri yake hii isitoke nje. "Wakati nakula hivyo, roho ya ibilisi ilikuwa ikinieleza kwamba kitu hiki ni kwa ajili yangu, kwamba hatakiwi yeyote kujua, vinginevyo nguvu itaondoka."
Joshua aliendeleza kwa kuelezea waumini na watazamaji duniani kote waliokuwa wakifuatilia matangazo hayo ya moja kwa moja kupitia kituo cha televisheni cha Kikristo cha Emmanuel TV kwamba kipande cha video kitaoneshwa kuthibitisha ungamo la Malomo.
Akielezea ilikuwa wazi mno kwake kuweza kushuhudia, aliziba uso wake na kushauri watazamaji wake wenye matumbo dhaifu kufanya kama yeye.
Kipande hicho cha video kinamuonesha Malomo akichanganya mkojo wake na kinyesi na kisha kunywa kwa kukera akionekana dhahiri kufurahia na kuburudika.
Waumini waliohudhuria walionekana wakitapika, kuhuzunishwa kwa kitendo hicho cha kujivunjia hadhi kutokana na mazoea hayo yaliyomkumba Malomo.
Kisha Joshua akawataka waumini kuungana pamoja kwa maombi na kuendelea kuomba 'shetani' atoke ndani ya Malomo! Alianguka sakafuni, mwili wa Malomo ukaanza kutetemeka ovyo.
Akielezea kilichokuwa kinaendelea, Malomo alisema alihisi kama kuna kitu kilikuwa kinatoka mwilini mwake.
Ndipo Joshua alipomuamuru Malomo kwenda kwenye vyoo vya kanisani hapo kuona kama hamu yake dhidi ya uchafu wa binadamu imebadilika kufuatia maombi hayo.
Harufu mbaya ya uchafu wa wenzake ilimsababishia Malomo mwenye kutapika. Alirejea kanisani, akishuhudia kwamba hamu yake ya hapo kabla imeondoka kabisa.
"Licha ya kusumbuliwa na harufu mbaya, ninaona haya, kwa hisia kwamba, inawezekanaje binadamu awe anakula kinyesi," aliwaeleza waumini, wakati akijiunga kucheza wimbo wa furaha wa Joshua.
SCOAN hadi sasa imesambaza kipande hicho cha video chenye utata kwenye mitandao ya kijamii ya YouTube na kupitia Facebook na kutazamwa na mashabiki zaidi ya 100,000 katika kipindi cha miezi minne tu.
Japo tatizo lililomkumba Malomo linaonekana kubwa zaidi, wengi wenye mazoea mabaya wamedai kuponywa kwenye kanisa la Joshua katika miezi michaxhe iliyopita, ikiwa ni pamoja na wale wenye mazoea ya kunywa mafuta ya taa, kula barafu, mchanga, makaa ya mawe, goroli na udongo.
T.B. Joshua katika miezi ya karibuni amewasha moto katika mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari, hususani kufuatia utabiri wake kuhusiana na kifo cha Rais wa Malawi, Bingu wa Mutharika na kuweka bayana uhusiano wake na viongozi wa Afrika kama John Atta Mills wa Ghana, Morgan Tsvangirai wa Zimbabwe na Rais mpya wa Malawi, Joyce Banda.
Kituo chake cha televisheni cha Emmanuel TV kimeendelea kujipatia umaarufu hususani ukanda wa Afrika ambako limekuwa si jina geni.