NYOTA WA KIKAPU ASHITAKIWA KWA KUIBA JINA...

Nyota wa mpira wa kikapu Kevin Durant anaelekea kupoteza jina lake maarufu la utani "Durantula" sababu mpiga gitaa anadai nyota huyo ameliiba kutoka kwake.
Durant ameshitakiwa jana kwenye Mahakama Kuu na mtu mmoja aliyejitambulisha kama Mark Durante, mpiga gitaa ambaye kwa mujibu wa hati ya mashitaka alikuwa maarufu sana miaka ya 1980 akipigia bendi za Public Enemy, The Aliens, The Next Big Thing na The Revolting Cocks.
Kwa mujibu wa hati ya mahakama iliyopatikana, ambayo Durante anasema nyota huyo alirithi jina "Durantula" alilokuwa akitumia katika 'maonesho yake stejini' na kulitumia kwenye soko lake la muziki, albamu, fulana, magitaa na bidhaa mbalimbali kama hizo.
Durante anadai ametuma barua kadhaa kwa watu wa karibu wa nyota huyo 'akiwataka kuacha kutumia jina hilo la utani' lakini anasema wawakilishi wa Durant walidai hakuwa akitumia jina hilo.
Katika mashitaka, Durante anadai Nike wametumia kuzindua kampeni yao ya viatu na Durant mwenyewe amesaini "Durantula" katika mikataba yake ya mpira wa kikapu ambavyo viko sokoni kupitia tovuti yake.
Mpiga gitaa huyo amesema alisajili nembo ya "Durantula". Anashitaki kutokana na madhara aliyopata na pingamizi kwa Durant kutumia jina hilo.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item