NYOTA WA SHOO YA "MOESHA" AFARIKI DUNIA...

Yvette Wilson, mmoja wa nyota wa "Moesha" amefariki akiwa na umri wa miaka 48 baada ya kupambana na maradhi ya saratani ya mlango wa kizazi, imeelezwa.
Yvette, ameigiza kama Andell Wilkerson ambaye ni rafiki wa Moesha, katika sizoni zote 5 mfululizo za shoo hiyo inayotikisa, na alicheza sehemu kama hiyo kwenye shoo ya "The Parkers."
Kansa ya Yvette ilikuwa katika hatua ya nne wakati akifariki.
Nyota mwenzake katika "Moesha", Shar Jackson amesema katika ujumbe wa mtandao wa Tweeter akisema, "Ooh Mungu, Moyo wangu umenyong'onyea kwa kutoamini. Nachukua nafasi hii kuwashukuru marafiki zangu wa mtandao huu kwa sala zao lakini Mungu akachagua kumchukua dada yangu Yvette katika ufalme wake."

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item