RAIS HOSNI MUBARAK AFARIKI DUNIA...


Mapigo ya moyo ya aliyekuwa Kiongozi wa Misri, Hosni Mubarak yamesimama. Yuko katika dakika za mwisho, anapumua kwa msaada wa mashine.
Mubarak, ambaye ameiongoza nchi hiyo kwa miaka 30 mpaka alipoondolewa madarakani katika mapinduzi yaliyokumba nchi za Kiarabu mwaka jana, alithibitishwa kuwa amekufa na madaktari wake tangu Juni 19, mwaka huu, kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na vyanzo vya hospitalini hapo.
Kiongozi huyo mwenye miaka 84 alihukumiwa kifungo cha maisha jela mapema mwezi huu.
Wajumbe wa Baraza la Kijeshi wamesema Mubarak hakufa, lakini yuko katika hali mbaya.
Maofisa Usalama wameeleza: Mubarak amewekwa kwenye mashine ya kupumulia baada ya moyo wake kusimama kufanya kazi wakati alipowasili kwenye hospitali ya kijeshi.
Umati mkubwa umekusanyika pamoja kwenye Uwanja wa Tahrir, kuna taarifa za kukanganya kuhusu hali ya Rais huyo wa zamani.
Maofisa kadhaa wa juu Misri sasa wanakanusha taarifa za Shirika la Habari la nchi hiyo kwamba Rais Hosni Mubarak 'amefariki dunia.' Wakinukuu vyanzo vya habari hospitalini, Shirika la Habari la MENA linaloendeshwa na serikali liliripoti kwamba Mubarak amethibitishwa kufa baada ya kupokelewa hospitali ya kijeshi Jumanne jioni.
"Mapigo ya moyo wa Mubarak yamesimama na yamejaribiwa kushituliwa kwa mashine maalumu mara kadhaa bila mafanikio," taarifa ya MENA imeeleza.
Hata hivyo, maofisa wa juu, wakiwamo viongozi wa kijeshi sasa wamekuwa wakijikanganya na ripoti ya awali. Jenerali Mamdouh Shahin, mfuasi wa Baraza Kuu la Kijeshi, wameripotiwa kuieleza CNN kwamba Mubarak "hakufa kama ilivyotangazwa, lakini afya yake imekuwa ikizorota na yuko katika hali mbaya."

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item