RAPA WILL.I.AM ADAKWA AKITANUA NA GARI LISILO NA NAMBA...

Rapa Will.i.Am amepoteza kwa muda gari lake aina ya DeLorean baada ya polisi kumshusha mjini Los Angeles wiki hii na kulikamata gari hilo, imeelezwa.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, polisi walimshusha garini rapa huyo Alhamisi usiku baada ya kugundua hana vibao vya namba za gari hilo. Walipotazama nyaraka, imeelezwa pia kwamba polisi waligundua matatizo kwenye usajili wake, hivyo kumshusha na kulikamata gari.
Imeelezwa kwamba Will alitoa ushirikiano mzuri wakati wote wa zoezi hilo. Will kisha akaondoka eneo la tukio kwa gari la rafiki yake.
Gari hilo litashikiliwa hadi Will.i.Am atakapoweka sawa nyaraka zake katika utaratibu unaotakiwa.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item