'MIZIMU' YAMPA KIBURI RAIS ASSAD NCHINI SYRIA...

Hawa ni 'Mizimu' ya kutisha inayochochea mauaji ambayo inaaminika kuwa ndio inampa kiburi Rais katili wa Syria, Bashar Assad kuendelea kung'ang'ania madarakani.
Wakiwa wamejichora tattoo mwilini zenye sura ya kiongozi wao, mizimu-watu hao wanalaumiwa kulitumbukiza taifa hilo kwenye mauaji wa halaiki ya watoto na wanawake kwa kuwachinja au kuwapiga risasi.
Wakiwa wameshika bunduki aina ya AK-47 na mapanga, wanasemekana kutekeleza kazi chafu ya serikali ambayo hata hivyo maofisa wanakanusha ghasia hizo kufadhiliwa na serikali.
Wakifahamika kwa jina la 'Shabiha', kwa maana ya 'Mizimu', wanavaa suari za kijeshi na fulana nyeusi huku wakilipwa kiasi cha Pauni za Uingereza 130 kwa siku.
Mbinu zao za kufanya kazi ni kurandaranda mijini baada ya majeshi kusimamisha mashambulizi. Chanzo cha habari kimesema: "Mpango wao ni kuijengea hofu jamii kubwa ya raia wa kawaida na kuchochea uondoaji ukabila."
Mauaji ya halaiki ya wananchi 108 mjini Houla wiki mbili zilizopita, wakiwamo watoto 49, yameshutumiwa na kundi ambalo limebobea kwenye dini la Muslim Alawite sect.
Wameripotiwa pia kuwapiga risasi na kuwaua wafanyakazi 12 mjini Qusayr na wanakijiji 78 huko Qubair wiki iliyopita.
Dk. Mousab Azzawi, amabye anaendesha Mtandao wa Syria wa Haki za Binadamu kutoka London lakini ambaye amewahi kuwatibia baadhi ya wafuasi wa Shabiha mjini Latakia, alisema hivi karibuni: "Walikuwa kama madubwana.
"Walikuwa na misuli mikubwa na matumbo makubwa na madevu. Walijidunga sindano maalumu kuvimbisha miili yao. Nililazimika kuongea nao kama mtoto maana wanapenda sana watu wenye upeo mdogo wa kufikiri.
Wanaharakati nchini Syria wanakadiria zaidi ya watu 13,000 wamekufa tangu kuanza harakati za kudai mabadiliko dhidi ya vikosi vya Serikali ya Syria zilizoibuka miezi 15 iliyopita na kusababisha umwagaji mkubwa wa damu.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item