AMREKODI MAMA YAKE AKITEMBEA USINGIZI NA KUSAMBAZA KWENYE INTANETI...



Baada ya miaka ya kuandaa chakula, kufua nguo chafu na kupeleka watoto kwenye mazoezi ya soka, mama wengi wanastahili heshima japo kidogo.
Lakini moto huyu aliyekosa fadhila amemshukuru mama yake kwa kumpiga picha za video akitembea huku akiwa usingizini na kuituma kwenye mtandao wa intaneti.
Video hiyo yenye mpwitompwito, iliyowekwa kwenye mtandao wa YouTube, inaonesha mama huyo aliyevalia pajama akirandaranda jikoni, huku mtoto wake wa kiume akimfuatilia na kamera yake.
Kijana huyo, ambaye ambaye anatumia jina la 'stillsoundlyawake', kisha akahoji "ni kitu gani hasa unachofanya mama."
Huku macho yakiwa wazi na kuzungumza kwa umakini, mama huyo ameeleza kwamba alikuwa akijaribu kufungua 'uzio wa nyanya' - aina ya waya unaotumika kukuzia miti ya nyanya.
"Ni namba maalumu," alisema. "Nilikuwa nafanya kitu maalumu. Lakini uzio wa nyanya haukufunguka."
"Sehemu nyingine," alisema. "Nilijaribu vitu vingi. Lakini haikuweza kufunguka na naondoka sasa."
Baada ya mwisho, na kipekee mno, kucheza huku akitembea, mwanamke huto kisha akatoka jikoni, akidhaniwa kuwa alielekea tena kitandani kulala.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item