ASKARI ALIYEMLIPUA MWANDISHI DAUDI MWANGOSI APANDISHWA KIZIMBANI...

                   BREAKING NEWS!!                
Askari anayetuhumiwa kumuua mwandishi Daudi Mwangosi (kushoto) anaonekana akijiandaa kufyatua bomu.
Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kwamba askari polisi aliyemlipua kwa bomu mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Daudi Mwangosi na kumuua amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya mkoani Iringa muda mfupi uliopita kujibu mashitaka ya kuua kwa kukusudia.
Askari huyo mwenye miaka 23 aliyetambuliwa kwa jina la PC Pacificus Cleophas Simon alifikishwa mahakamani hapo huku akiwa kazingirwa na maofisa usalama takribani saba na hivyo kuwapa wakati mgumu waandishi wa habari kuweza kupata picha yake.
Kutokana na utaratibu wa kesi za mauaji, askari huyo mwenye namba za kipolisi 2573 hakutakiwa kujibu chochote na kurejeshwa tena rumande kutokana na kunyimwa dhamana hadi kesi yake itakapotajwa tena Septemba 26, mwaka huu. Upelelezi kuhusu mauaji hayo bado haujakamilika.
Imefahamika kwamba hivi karibuni, askari wote walioonekana kwenye ushahidi wa picha wakimshambulia marehemu Mwangosi walikamatwa na kuhojiwa kuhusiana na mauaji hayo. Baada ya kuhojiwa ndipo ikabainika kuwa Pacificus ndiye alikuwa mhusika mkuu wa kumlipua marehemu kwa bomu la machozi.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item