CHEKA TARATIBU...

Mzee mmoja alikuwa na matatizo makubwa ya kusikia kwa miaka kadhaa. Akaamua kwenda kwa daktari na kwa bahati nzuri akafanikiwa kuwekewa kifaa maalumu kilichomsaidia kuweza kusikia kwa asilimia 100.
Baada ya mwezi mmoja mzee yule akarejea kwa daktari. Daktari akamkumbuka na kumuuliza, "Usikivu wako sasa uko safi kabisa. Familia yako lazima watakuwa wamefurahi kuona sasa unaweza kusikia tena."
Yule mzee akajibu kwa unyonge, "Oh, sijamweleza yeyote pale nyumbani kwa sasa. Nilipofika nikakaa kando na kusikiliza majadiliano yao. Nimebadilisha wosia wangu mara tatu!!" Duh...

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item