'KIPANYA' CHAFYEKA ABIRIA 13 BUTIAMA...
https://roztoday.blogspot.com/2012/09/chafyeka-abiria-13-butiama.html
Watu 13 wamekufa na wengine 14 kujeruhiwa katika ajali ya gari katika kijiji cha Mkiringo wilayani Butiama mkoani Mara.
Ajali hiyo ilitokea juzi jioni wakati gari hilo aina ya Toyota Hiace namba T 123 CAE likitoka mjini hapa kwenda Nyamuswa, Butiama. Lilikuwa likiendeshwa na Emmanuel Joseph ‘Diouf’.
Mashuhuda wa ajali hiyo walisema gari hilo lilikuwa katika mwendo mkali huku likiwa limebeba abiria kupita kiasi.
Walieleza kuwa gari hilo lilipasuka tairi la nyuma kulia na kupinduka huku likiviringika mara tatu na kusababisha vifo na majeruhi 14 waliolazwa katika hospitali ya mkoa wa Mara sambamba na maiti hao.
Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk Samson Winani aliwathibitishia waandishi wa habari kupokea majeruhi na maiti.
Dk Winani alitaja maiti 12 waliotambuliwa na ndugu zao kuwa ni Diouf, Pendo John (39) na mtoto wake Joseph Richard (5) wakazi wa Bisarye, Razak Shaabani, Hamis Kanyoro, Nyamazore John, Innocent Kweka na Jihadhari Dogori wakazi wa Nyamuswa.
Wengine ni Isaack Hassan, Makuli Maguri na wengine wawili waliotambuliwa kwa jina moja moja; Masoke na Richard wakazi wa Butiama.
Dk Winani alitaja majeruhi wa ajali hiyo wanaoendelea na matibabu huku hali zao zikiendelea vizuri, kuwa ni Nyamakunguru Fanuel, Nyamazege Warioba, Gosbert Waryoba, Hamisi Wisaka, Hamisi Gibombi na Hamis Nyaga.
Majeruhi wengine ni Mganda Nyamajege, Efrancia Kiamanzi na Beatrice Siriwa ambao ni wanafunzi wa sekondari ya Chief Ihunyo waliokuwa wakitoka Dar es Salaam kurudi shuleni.
Wengine ni mwalimu wa shule ya msingi Butiama B, Beatrice Komba ambaye amevunjika mguu, Bunuli Madube na mtoto wa miaka minane, Martha Makuli ambaye baba yake amekufa katika ajali hiyo.
Kutokana na ajali hiyo, wananchi mkoani Mara wamelilaumu Jeshi la Polisi kwa kushindwa kusimamia ujazo wa abiria kwenye magari kabla ya kuanza safari na kusababisha vifo ambavyo vinaweza kuepukwa.
Mmoja wa wananchi katika stendi ya Nyasho alisema alishuhudia gari hilo likianza safari ya Butiama likiwa limejaza abiria kupita kiasi huku Jeshi la Polisi likishindwa kuchukua hatua.
"Nililishuhudia likianza safari huku limejaza sana na sehemu ya mbele ambapo hutakiwa kukaa abiria wawili walikuwa wane," alisema mwananchi huyo ambaye hakupenda kutajwa jina gazetini.
Alisema haoni kazi inayofanywa na askari wa usalama barabarani ikiwa wanashindwa kusimamia majukumu yao ipasavyo na lawama zote za ajali hiyo zinapaswa kuelekezwa kwao.