CHEKA TARATIBU...
https://roztoday.blogspot.com/2012/09/cheka-taratibu_9.html
Siku moja mwanamke alikuwa akiendesha gari lake kwenye barabara kuu. Mara kwa mara alikuwa akitazama spidi mita yake kuhakikisha hazidishi mwendo unaoruhusiwa kisheria. Hatahivyo, alipotazama kwenye kioo cha pembeni akaona kuna gari la polisi likimfuatilia. Mbaya zaidi lile gari la polisi likawasha king'ora chake. Akaanza kujiuliza mwenyewe, "Nimefanya kosa gani Mungu wangu? Mkanda nimefunga, naendesha mwendo wa kawaida tu, sijakunywa pombe, leseni na nyaraka zote ninazo!"
Basi akaamua kuegesha gari lake pembeni na polisi nao wakaegesha upande mwingine wa barabara. Akawa kajiandaa kwa kulipishwa faini. Polisi alipofika karibu, mwanamke akashusha kioo na kuelekeza vidole vyake masikioni na kutingisha kichwa chake akimaanisha ni kiziwi. Polisi akatabasamu, kwakuwa alikuwa akifahamu lugha ya ishara, na kumjibu, "Nafahamu. Nimekusimamisha ili kukueleza kwamba honi ya gari lako imenasia, inalia muda wote!" Ebo...

Thank you, I have recently been looking for facts about this question for a while and yours is the best I have found so far.
ReplyDelete