WATU WACHOMWA KAMA MISHIKAKI NCHINI SYRIA...

KUSHOTO: Mmoja wa walionusurika katika mlipuko huo akikatiza katikati ya wingu jeusi la moto. JUU: Watu watatu waliouawa katika mlipuko huo wakifanya usafi muda mfupi kabla tukio lililokatisha uhai wao. CHINI: Muda mfupi baada ya kutokea mlipuko.
Picha za kushangaza zinaonesha tukio la kutisha tanki la mafuta la serikali likilipuka na kuua wapiganaji wa kundi la waasi kwenye mji wa Aleppo, uliokumbwa machafuko nchini Syria.
Mfululizo wa picha za kujirudirudia zinaelezea simulizi la kuhuzunisha, kwanza zinaonesha eneo la mtaa tulivu, kisha tukio la kutisha la lori la mafuta likiwasili na kisha kufuatiwa na mlipuko mkubwa.
Picha hizo zenye nguvu, ambazo zinang'arisha mwanga mkali juu ya ukatili katika maishaya kila siku kwa watu wa Syria chini ya uongozi wa majeshi yanyomtii Rais Bashar Assad, zilipigwa na Tracey Shelton, mwakilishi wa Global Post.
Shelton aliandika kuhusu uzoefu wake wa kupigapicha, akielezea jinsi alivyotumia muda kuweka kambi na wafuasi wa batalioni ya Noor Den al-Zenke watu walioweka vizuizi mitaani ambao sasa wanaunda mstari wa mwisho wa mapambano kati ya vikosi vya serikali na vikosi vya upinzani.
Alifafanua jinsi katika shambulio hilo la asubuhi, watu hao walivyokuwa wamepumzika na kutaniana huku wakifanya usafi eneo hilo baada ya shambulio la lori la mafuta siku ya jana yake.
Wakati wa shambulio hilo, lori hilo la mafuta halikuchukua muda kulipuka, alielezea. Lakini safari hii, shambulio la ghafla liliwashitusha na kuua watu watatu.
Shelton alifafanua kutoka moyoni mwake jinsi walivyokimbia kutoka katika wingu jeusi la moto na kusubiri wengine watoroke kutoka katikati ya mabaki ya nyumba.
"Huku wingu la moshi wa moto likifunika mtaa tulikimbia kurudi na katika nanmna ya kuudhi tukasubiri wengine watoroke kupitia kwenye wingu hilo la moto na mabaki ya nyumba. Lakini hakuna aliyekuja. Katika mlipuko huo wa pili, watu watatu walivunjika, kupoteza damu nyingi," aliandika.
Picha hizo za kuhuzunisha zimekuja huku Taasisi ya Ufuatiliaji Haki za Binadamu Syria yenye makao yake Uingereza imekadiria kuwa zaidi ya watu 26,000 wameuawa nchini humo tangu kuanza kwa machafuko Machi, mwaka jana - zaidi ya theluthi mbili ikiwa ni wananchi wa kawaida.
Imekuwa wiki nyingine ya vifo kwa wakazi wa Aleppo huku majeshi ya serikali yakifanya mashambulio makali ya anga Jumatatu.
Mkazi mmoja amesema shambulio hilo lilifanywa na majeshi ya serikali ya Syria katika eneo lenye wakazi wengi la jiji hilo na kwamba mapigano zaidi talifuatia.
Inaaminika kwamba katika moja ya mashambulio makubwa zaidi wiki hii, watoto saba waliuawa.
Waasi walipata ushindi mkubwa Ijumaa jioni pale walipoteka sehemu ya kambi za jeshi za Hanano, moja ya ngome kubwa ya jeshi hilo, mwanaharakati alisema.
Taasisi ya Ufuatiliaji Haki za Binadamu Syria ilisema waasi walikuwa na uwezo wa kufika ukingoni mwa kambi za jeshi, ambako wamewaweka zaidi ya wanajeshi 2,000 wakiwamo wengi waliochukuliwa kutoka sehemu nyingine za Syria.
Mwanaharakazi wa Aleppo, Mohammed Saeed alisema waasi walikuwa na uwezo wa kuwaachia mateka kutoka kambi za jeshi zilizotapakaa, ambazo ziko karibu na katikati ya mji huo.
Waasi pia walishambulia kitovu cha ukaguzi cha kijeshi kinachounganisha Aleppo na Uturuki, ambako watu wengi wa Syria wawekwa ukimbizini kutokana na mapigano hayo. Waangalizi walisema waasi sita waliuawa katika shambulio hilo.
Waangalizi na kundi jingine la wanaharakati linalofahamika kama Tume za Ndani za Uratibu pia zimeripoti mapigano mapya mjini mji wa Tadamon ambao uko jirani na Damascus, wakidai helikopta ya jeshi ilitunguliwa.
Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria vimeshuhudia vikichukua sura mpya Agosti pale majeshi ya Assad kuanza kutumia nguvu za kijeshi kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa machafuko hayo. Ndege kadhaa za kivita na helikopta zimetunguliwa kwa wiki kadhaa zilizopita.
Mapigano hayo pia yamefika katika mji wa Aleppo, ambao umekuwa tulivu kwa miezi yote 18 tangu kuanza kwa machafuko hayo.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item