MAMA ALIYEKOSA AIBU AMTETEA HADHARANI KIJANA WAKE MBAKAJI...

KUSHOTO: Joseph Moran. JUU: Sarah Moran, mama wa Joseph akiwa nje ya mahakama na mabango ya kumtetea kijana wake. CHINI: Basi la mwisho ambalo dereva wake alimkataa mwanafunzi kwa kupungukiwa Senti 20 tu.
Kijana wake alimpiga na kumbaka mwanafunzi wa sheria ambaye alikuwa ameachwa kituoni na basi la mwisho akiwa njiani kurudi nyumbani kutokana na kupungukiwa Senti 20 tu katika nauli ya Pauni za Uingereza 5.
Lakini Sarah Moran hakuonesha aibu yoyote au kujutia kwa yale aliyofanya kijana wake Joseph ambaye alihukumiwa kifungo cha maisha jana kwa kosa la shambulio la 'kinyama na kutisha'.
Aliandamana nje ya mahakama huku akiwa kavakia fulana yenye picha ya kijana wake huyo mwenye miaka 19 ikiwa na maneno yanayosomeka 'hana hatia' na kubeba mabango. Alisisitiza amehusishwa kimakosa na tukio hilo.
Sarah, ambaye aliwasili katika Mahakama Kuu ya Nottingham akiwa amefuatana na rafiki wa kike wa kijana wake pamoja na wanafamilia kadhaa na marafiki, alisema kipimo cha DNA kilipatikana eneo la tukio kwa sababu tu alikuwa akitokwa na damu kwenye mkono wake.
Alijikwaa tu mbele ya msichana huyo katikati ya mji wa Nottingham majira ya saa 9:30 alfajiri ya usiku mmoja wa Desemba, mwaka jana na alihitaji msaada wa msichana huyo, aliendelea kushikilia msimamo wake mama huyo.
Jaji alimbatiza jina kijana wake huyo 'mwongo' kwa kushikilia hadithi hiyo wakati wote wa kesi hiyo.
Ukweli ni kwamba, Joseph alimvamia msichana huyo baada ya kuwa ameachwa akiwa hajui la kufanya kwenye giza.
Katika mfano wa kufadhaisha wa kukosa ubinadamu nchini Uingereza, msichana huyo mwenye miaka 23 hakuruhusiwa kabisa kupanda basi hilo la mwisho kwenda nyumbani sababu alikuwa kapungukiwa Senti 20 katika nauli yake.
Picha za kukera zilizonaswa na kamera za CCTV zilionesha msichana huyo akimsihi derva kwa saidi ya dakika nane, huku abiria wake wakimkodolea macho bila kutoa msaada wowote.
Msichana huyo alilazimika kumpigia simu mama yake kumwomba aje kumchukua na kuanza kutembea kuelekea upande ambako mama yake angetokea.
Lakini, baada ya kusafiri kwa umbali usiozidi maili moja, alivamiwa na Joseph, ambaye alikuwa amelewa na kuvuta bangi, akamkokota ndani ya bustani na kumbaka katika shambulio lililochukua dakika 25.
Baada ya kupatikana na hatia ya kubaka na kujeruhi kwa kukusudia, Joseph alihukumiwa adhabu hiyo ikiwa na lengo la kuilinda jamii.
Huku akichezea vidole vyake na kunyoosha mikono yake kizimbani, alielezwa kwamba lazima atumikie kifungo cha miaka sita na nusu gerezani kabla ya kuanza kufikiriwa kuachiwa huru.
Ataachiwa huru tu endapo atathibitika kuwa si hatari tena kwa jamii.
Msichana huyo mwenye miaka 23 aliwashukuru wote waliohusika katika kumfikisha mahakamani mtuhumiwa wake katika taarifa aliyoitoa kupitia kwa polisi.
Alisema: "Kwanza kabisa napenda kuishukuru familia yangu kwa msaada mkubwa na sala wakati wote nilipokuwa napitia katika wakati mgumu sana.
"Ningependa pia kuwashukuru wafanyakazi wa Kituo cha Afya cha Queen kwa kujitolea, uweledi, matunzo na kujali walikonionesha katika wiki niliyokaa hospitalini hapo na wiki zilizofuatia wakati nikienda kwa matibabu zaidi.
"Polisi hawakufanya kazi kwa bidii tu katika kesi hii, pia wameonesha hisia kali juu yangu, kitu mabacho wakati mwingine kinaweza kisionekane kwa urahisi. Kwa hilo napenda sana kuwashukuru mno.
"Sasa nasonga mbele na maisha yangu na nataka watu waheshimu hilo na kuacha kutusumbua mimi na familia yangu."
Jaji James Sampson alisema Joseph amefanya shambulio la 'kinyama na kutisha' na hakuonesha hata chembe ya kujutia au aibu kwa kitendo alichofanya.
Hadi kufikia takribani mwaka mmoja kabla ya shambulio hilo, Joseph alikuwa akiishi eneo la uswahilini huko Sneinton pamoja na mama yake.
Jirani mmoja alisema: "Kwa mama kama yule, Joseph hawezi kurekebishika."

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item