AELEZA ALIVYONUSURIKA KUFA KATIKA NDEGE YA EASYJET...

KUSHOTO: Ndege ya EasyJet. KULIA: Annette Townend akionesha kikaratasi cha kuomba msaada.
Mgonjwa wa saratani amevumilia mateso ya kutisha akiamini kwamba anaelekea kufa baada ya kunyimwa oksijeni katika ndege aliyopanda akielekea mapumzikoni nchini Cyprus, amedai.
Annette Townend mwenye miaka 56, anasema alichelewa kupanda ndege ya Shirika la EasyJet na kuhema kwa shida baada ya kuwa amezuiwa kutumia kiti cha magurudumu.
Muda mfupi baada ya kuruka, alimweleza mhudumu 'oksijeni, oksijeni', na kuishia kutaarifiwa kwamba 'ipo kwa ajili ya dharura pekee'.
Alichanganyikiwa mno baada ya kubanwa na pumu ndipo akaandika kwa haraka ujumbe 'nashindwa kupumua nahitaji oksijeni nakufa' kwenye kipande cha karatasi na kukipachika kwenye kiti cha pembeni yake.
Ukiacha mwanamke mlemavu nyuma yake, anasema hakuna yeyote aliyeonesha kujali hali yake mbaya.
Aliendelea na mateso hayo kwa muda wote wa masaa manne na nusu ya safari hiyo kutoka Manchester, lakini anasema aliachwa kwatika hali kama hiyo na kuishia kulazwa hospitali akisumbuliwa na nimonia.
Akikumbukia mateso hayo, alisema: "Nilikuwa nikikaribia kufa kwa kukosa hewa, sikuweza kuhema na sikuwahi kuwa katika mashaka makubwa kama vile hapo kabla. Hakika nilihisi kabisa naelekea kufa. Kadri ndege ilivyozidi kupaa juu nilishindwa kabisa kupumua.
"Madaktari wangu walinieleza baadaye nilikuwa na bahati kuwa hai. Mtazamo wa wahudumu wa EasyJet ulikuwa wa kukera."
Shirika hilo la ndege limetupilia mbali malalamiko hayo, likidai Annette alikataa msaada wa kiti cha magurudumu katika uwanja wa ndege na alikubaliana kusafiri bila oksijeni.
Hatahivyo, mjane huyo, ambaye anamiliki biashara ya udobi. amechukizwa na amedhamiria kuchukua hatua za kisheria.
Annette anayeishi Baildon, huko West Yorkshire, amekuwa akifanyiwa tibakemikali kwa ajili ya saratani ya matumbo na aliamini kwamba safari yake hiyo ya siku kumi kusalimia marafiki nchini Cyprus ingemsaidia kupata nafuu.
Lakini kuchelewa kwa dakika 15 kulikosababishwa na maofisa usalama kukagua mzigo wake wa mkononi ulisababisha alipokwenda kwenye dawati kupata msaada wa kiti cha magurudumu, asikute yeyote pale.
Alilazimishwa kutembea kukatisha uwanja, huku akikokota begi lake nyuma.
Alisema alipandwa na 'jazba' wakati jina lake lilipoitwa katika kipaza sauti kwa haraka kuelekea katika lango kuu.
"Nilikuwa nikikoroma, kushindwa kupumua na hasira pale nilipofika na ndege ilikuwa imechelewa kwa dakika kumi sababu ilinichukua muda mrefu," alisema.
"Niliandika ujumbe wakati abiria wa nyuma yangu aliponiuliza nina tatizo gani. Wale wahudumu walitakiwa kuwa wameona kwenye kiti lakini hawakuchukua hatua zozote."
Msemaji wa shirika hilo la ndege alisisitiza juzi kwamba mfanyakazi wa 'msaada maalumu' alimchukua Annette kutoka eneo la maduka la uwanja huo wa ndege ambako alikuwa katika wakati mgumu.
Aliongeza: "Kipaumbele kikubwa kabisa cha EasyJet ni afya na usalama wa wote waliomo kwenye ndege. Wafanyakazi wetu katika ndege waliongea na Annette kwa kina kuhakikisha yuko vizuri na kukubaliana naye kwamba anamudu kuendelea na safari bila kuhitaji oksijeni.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item