BEKI WA CHIEFS AMUUA MPENZI WAKE NA KUJIUA KWA RISASI...

Mapema jana Jumamosi asubuhi, mlinzi wa timu ya Chiefs Jovan Belcher amempiga risasi na kumuua rafiki yake wa kike mwenye miaka 22, Kasandra Perkins katika nyumba iliyo karibu na jengo la timu. Wapenzi hao walikuwa na binti wa miezi mitatu ambaye kwa sasa yuko katika mikono salama ya ndugu.
Polisi walisema kwamba Jovan na Kasandra waliingia katika malumbano majira ya Saa 1:00 asubuhi ya Jumamosi. Jovan alimpiga risasi Kasandra mara kadhaa. Alikimbizwa katika hospitali ya jirani ambako alitangazwa kuwa amefariki.
Baada ya kupigwa risasi, Jovan aliendesha gari lake kwenye eneo lililo karibu na makao makuu ya timu na kujiua. Wafanyakazi wa timu walijaribu kumzuia Jovan asichukue hatua yoyote ya vurugu kabla ya mchezaji huyo kujielekezea mwenyewe mtutu wa bunduki.
Mama wa Kasandra aliwapigia polisi baada ya kushuhudia tukio hilo na kuwaeleza kwamba binti yake amepigwa risasi. Polisi waliwasili eneo la tukio na kumkuta Jovan kwenye maegesho ya magari akiwa na kunduki yake kichwani. Wakati ofisa mmoja akishuka kutoka kwenye gari lake alisikia mlio wa bunduki. Jovan baadaye alitangazwa kuwa amefariki.
Meneja Mkuu wa Chiefs, Scott Pioli na Kocha Mkuu, Romeo Crennel walikuwa miongoni mwa waajiriwa wa timu hiyo katika eneo la tukio hilo.
Jovan aliripotiwa kuwashukuru Crennel na Pioli kwa yote waliyomfanyia, na kisha kujiua.
"Pioli na Crennel na kocha mwingine au mwajiriwa walikuwa wamesimama nje na kuonekana wakizungumza naye. Ilionekana walikuwa wakizungumza na mtuhumiwa," Msemaji wa Polisi wa Jiji la Kansas, Darin Snapp alisema.
"Mtuhumiwa huyo alianza kuelekea upande tofauti na makocha hao na maofisa hao na ndipo waliposikia mlio wa bunduki.
"Walisema mchezaji huyo alikuwa akiwashukuru kwa kila kitu walichomfanyia. Walikuwa akiongea naye tu na alikuwa akiwashukuru na kila kitu. Hapo ndipo alipoondoka na kujipiga risasi mwenyewe."
Wachezaji wa Chief walitakiwa kujikusanya eneo la timu hiyo ili kuweza kupewa taarifa ya kila kitu.
"Familia nzima ya Chiefs imehuzunishwa mno na tukio la leo, na tunatuma salamu za rambirambi na sala kwa familia na marafiki walioathiriwa na janga hili lisilofikirika," Mwenyekiti wa timu na Ofisa Mtendaji Mkuu, Clark Hunt alisema katika taarifa.
Chiefs imepangwa kucheza na Carolina Panthers kwenye uwanja wa Arrowhead leo, na kwa mujibu wa Joseph Person wa Charlotte Observer, Panthers wameambiwa na wasimamizi wa ligi kusafiri hadi Jiji la Kansas kama vile mechi hiyo itachezwa.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item