UJENZI WA MIUNDOMBINU KUAJIRI 240,000 MWAKA UJAO...

Jumanne Sagini.
Programu ya Usafiri ya Serikali za Mitaa Awamu ya Pili (LGTP 2) inayotarajia kuanza Julai mwakani, itatoa ajira kwa Watanzania 240,000 wakati wa utekelezaji wake.
Ajira hizo zitazalishwa kupitia makandarasi  wazalendo ambao watapewa nafasi ya utengenezaji wa miundombinu.
Akizungumzia katika mkutano wa siku moja kuhusu Programu hiyo, Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Jumanne Sagini  alisema ajira hizo zitazalishwa kutokana na miradi ya ujenzi na matengenezo ya miundombinu.
Alisema Serikali itahakikisha utekelezaji wa programu  hiyo unafanikiwa na kusisitiza kuwa mafanikio yake yatakuwa katika kuongeza barabara bora na ajira kwa Watanzania.
Sagini alisema ili kupunguza gharama za uendeshaji programu hiyo Serikali itatumia makandarasi  wazalendo watakaoajiri wafanyakazi wa ndani.
 “Mafanikio ya programu hii ya pili ni pamoja na kuongeza barabara nchini pamoja na ajira zitakazopatikana kwa kutumia programu hii” alisisitiza  Sagini.
Akizungumza kwa niaba ya wadau wa maendeleo katika sekta ya miundombinu ,Mkuu wa Miundombinu kutoka  Shirika la Kimataifa la Ushirikiano wa Kimaendeleo la Japan (JICA) Yuzulu Ozeki alisema wadau hao wamefurahishwa kuona kuna programu maalumu kusaidia uwekezaji makini katika maendeleo ya barabara hasa za vijijini.
Akiwasilisha mada katika Mkutano huo, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Miundombinu katika Wizara hiyo Elina Kayanda aliwashukuru washirika wa maendeleo na kusema ni matumaini yake kwamba wataendelea kusaidia kufanikisha programu hiyo.
Programu hiyo inatarajia kutumia zaidi ya dola za Marekani milioni 772 ambapo dola milioni 240 sawa  na asilimia 31 zitatoka kwa washirika wa maendekeo na Serikali kutoka Mfuko wa Barabara itatoa dola milioni 212 sawa na asilimia 27.
Programu hiyo imelenga kuwezesha barabara kadhaa kupitika mwaka mzima, kuondoa vikwazo,  kutengeneza barabara na  kutanua zaidi barabara za barabarani.
Awamu ya kwanza  ilianza Agosti 2007 ambapo barabara nyingi  kutoka asilimia  14 hadi 22 zilijengwa.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item