CHATU ANASWA AKIMEZA KONGONI MZIMA-MZIMA...
https://roztoday.blogspot.com/2012/12/chatu-anaswa-akimeza-kongoni-mzima-mzima.html
Hili ni tukio adimu la kushangaza pale chatu mkubwa anayepatikana barani Afrika aliponaswa na kamera akijaribu kula mwili wote wa kongoni.
Chatu huyo mkubwa alionekana macho yake yakiwa makubwa pale alipokutwa katika misitu wa Afrika Kusini akimeza mnyama huyo mkubwa.
Inadhaniwa kuwa ni mara ya kwanza tukio hili kunaswa kwenye kamera wakati chatu - ambaye anaweza kufikia urefu wa futi 16 - aliyeaminika kujaribu mawindo duni zaidi.
Tukio hilo la kutisha limepigwa picha kwenye Hifadhi ya Wanyama ya Welgevonden, Afrika Kusini na Meneja Rudi Hulshof.
Rudi mwenye miaka 35 alisema: "Hii ilikuwa mara ya kwanza kuweza kuona kitu kama hiki, na nimekuwa nikifanya kazi kama mwindaji katika hifadhi kwa miaka 15 hadi sasa katika Afrika Kusini, na nimeshasafiri pia katika nchi nyingine za Afrika.
"Hili ni tukio adimu la kushangaza kuweza kunaswa, na kwa uzoefu wangu ni mara ya kwanza kurekodiwa, kuweza mwenyewe kupigapicha na kuelezea jinsi chatu wa Afrika Kusini alivyokamata windo kubwa la kongoni wa bluu.
"Wataalamu nilioongea nao wote wamevutiwa na kupigwa bumbuwazi na picha hizo baada ya kuziona.
"Ni mara chache mno kwa chatu kukamata wanyama walio hai wanyonyeshao, lakini hii ingeweza kuhusisha wanyama wadogo kama sungura, panya n.k.
"Lakini kuweza kufanikiwa kitu kikubwa kama hiki inastaajabisha. Hii inaweza kuonesha jinsi gani chatu anahitaji kupanua mdomo wake kwa kiwango chake kujaribu kumeza kongoni huyo.
"Nimekuwa nikipiga picha wanyamapori kwa miaka 15 iliyopita wakati nikishughulika katika fani hii, kwenye hoteli tofauti za katika hifadhi zilizotapakaa kuzunguka Afrika Kusini."
Rudi anasema alilifuma tukio hilo lisilo la kawaida kwa bahati wakati akiwa anawatafuta simba na chui.