BRITISH AIRWAYS KUFYEKA WAFANYAKAZI 400...

Shirika la ndege la British Airways limepanga kupunguza wafanyakazi 400 wa kwenye ndege kati ya wafanyakazi wake 14,000.
Shirika hilo liko katika mazungumzo na chama cha wafanyakazi cha Unite kuhusu mipango yake hiyo na imetoa uhakika kwamba upunguzaji huo utafanyika kwa njia ya kustaafu kwa hiari.
Uamuzi huo utaathiri wale tu wanaofanya kazi katika safari zake ndefu au fupi pekee, na sio wale wanaofanya zote kwa pamoja.
British Airways imesema Jumanne imeshaanza majadiliano ya siku 90 na Unite.
Upunguzaji huo unatarajiwa kuongeza shinikizo katika shirika mama la International Consolidated Airlines Group, ambalo tayari linakabiliwa na migomo wa msimu wa mapumziko kwenye shirika lake la Iberia.
Ofisa wa Unite, Oliver Richardson alisema chama hicho kitafanya kazi kuhakikisha kwamba British Airways 'kulinda ahadi ya "hakuna kulazimishwa" kustaafu'.
"Jaribio lolote la kulazimisha watu wanaotaka kuendelea kufanya kazi British Airways kuwaondoa kazini litapingwa vikali," alisema.
British Airways linapigana na muendelezo wa mapambano kuhusu malipo na wafanyakazi ya mwaka 2010 na 2011 dhidi ya wafanyakazi wa kwenye ndege, ambayo yalisuluhishwa mwaka jana baada ya migomo kadhaa mfululizo.
Shirika lake dada la ndege, Iberia lilisema mapema mwezi huu litapunguza takribani ajira 4,500 ili kuweza kuinua ushindani. Mfululizo wa migomo unatarajiwa kuibuka mwezi ujao kupinga hatua hiyo.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item