CHEKA TARATIBU...
https://roztoday.blogspot.com/2012/12/cheka-taratibu_3.html
Baada ya kutokea ugomvi mkubwa kati ya kondakta wa daladala na Mmakonde mmoja, abiria wanaingilia kati na kusuluhisha. Kondakta akaendelea na kazi yake ya kuita abiria vituoni huku akiuliza wanaoshuka. Kufika maeneo ya Posta Mpya, kwa mshangao Mmakonde akamfuata Kondakta na kuanza kumtambia, "Na leo nimekukomesha. Kwa taarifa yako nilikuwa nashukia Manzese lakini kila ukiuliza wa kushuka mie nimebanisha tu. Ukome siku nyingine!" Kasheshe...