MTOTO WA AJABU ANAYEKUA VIUNGO MARA 50 KWA SIKU...
https://roztoday.blogspot.com/2012/12/mtoto-wa-ajabu-anayekua-viungo-mara-50.html
Mtoto mdogo wa kike aliyezaliwa na hitilafu kwenye viungo vyake amepata matumaini mapya kupitia upasuaji kadhaa wa kuokoa maisha yake.
Katie Renfroe mwenye miaka minne, aligundulika kuwa na matatizo kabla hajazaliwa, hivyo kusababisha baadhi ya viungo vyake usoni kukua isivyo kawaida.
Pia sehemu ya ubongo wake iliondolewa katika harakati za kudhibiti ukuaji huo ambao ulikuwa ukifanyika takribani mara 50 kwa siku.
"Tunachofahamu ni kwamba tunampatia mapenzi yetu yote, uangalizi wa karibu tunaoufahamu kumpatia," anasema mama yake Angie Renfroe.
"Hatukuwahi kumchukulia kama ana mapungufu."
Katie ni mtoto wa sita kwa Angie na Danial Renfroe kati ya watoto wanane, mmoja ambaye alikuwa sambamba na madaktari aliwaeleza kwamba Angie hangeweza kuwa na watoto wengine zaidi.
Katika ngwe ya tatu, madaktari walibaini maumbile yasiyokuwa ya kawaida kupitia kipimo chake cha ultrasound. Kichwa cha mtoto huyo kilikuwa na 'umbile lisiloeleweka,' wazazi wake walielezwa.
Katika miezi mitatu na nusu, mtaalamu aliwaambia wazazi wake kwamba kichwa cha Katie kilikuwa kikubwa mara tatu zaidi ya ukubwa wa kawaida.
Aliwatajia ukuaji usio wa kawaida wa Katie, lakini haikumaanisha kitu kwa wanandoa hao wa bara kutoka Paxton. Pia aliwaeleza maisha yake na maisha yao yatakavyokuwa.
"Alikuwa akijaribu kutusaidia kuelewa kwamba lazima atakuwa mboga," anasema Danial.
Mtaalamu huyo aliwaeleza warudi katika kipindi cha wiki mbili baada ya kuwa wameamua nini watakachofanya.
Wanandoa hao walikwenda nyumbani kutoka Hospitali ya Moyo ya Sacred iliyoko Pensacola. Mara baada ya kufika, Angie alikwenda chumbani kwao, akajitupa kitandani na kuanza kulia.
"Nilijaribu kupata picha jinsi gani tutakavyoweza kukabiliana na hili," alisema. Na kisha akapata jibu ana maamuzi kadhaa ya kuchagua.
"Unaweza kulala hapa, unaweza kulia au unaweza kuliacha hili kwenye mikono ya Mungu, ambako huko ndiko liliko tegemeo lake," Angie anakumbuka mawazo yake. Baadaye aliongea na Mungu.
"Kama umeamua niwe naye, nitamuinua na kumtunza vema kwa kadri ya uwezo wangu kwa kuwa tu umenikabidhi."
Baada ya kuwa ameridhika na uamuzi wake, akaongea na Danial.
"Nilimweleza, "Kama huwezi kulikabili hili - wanatueleza itatugharimu vibaya - nenda sasa," anasema.
Anakumbukia kumwangalia kama vile mwendawazimu. Hakuwa akienda kokote.
Katie alizaliwa kwa njia ya operesheni kwenye Hospitali ya Moyo ya Sacred Januari 28, 2008. Angie hakumbuki sana kuhusu kujifungua isipokuwa 'mashavu makubwa' ya binti yake huyo.
Na tangu kufanya maamuzi yake hayo kuendelea na ujauzito wake miaka mitano iliyopita, kamwe hakutazama nyuma tena.
"Ni mtu ninayeamini," anasema. "Kama Mungu anakupa kitu fulani, usikitupe."