NSSF KUBADILISHA KABISA SURA YA DAR ES SALAAM...

https://roztoday.blogspot.com/2012/12/nssf-kubadilisha-kabisa-sura-ya-dar-es.html
![]() |
Muonekano wa katikati ya Jiji la Dar es Salaam ulivyo sasa katika picha iliyopigwa kwa juu. |
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), linakusudia kubadilisha kabisa sura ya baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam, kwa kujenga majumba ya kisasa ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Shirika katika kuhakikisha Jiji linaondokana na makazi holela.
Aidha, linakusudia kujenga bandari ya nchi kavu kwa lengo la kupunguza msongamano wa makontena bandarini, na pia kuiongezea uwezo bandari ili itanue wigo wa kupakia na kupakua mizigo kwa lengo la kuongeza kasi ya kuinua uchumi wa nchi.
Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa NSSF, Yacoub Kidula wakati wa semina ya Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini na Uongozi wa Shirika hilo iliyofanyika katika Hoteli ya Sea Cliff iliyopo Mangapwani, Zanzibar.
Akizungumzia makazi holela, Kidula alisema shirika limejipanga kuhakikisha Dar es Salaam inaondoka na makazi holela na kuupanga mji kisasa zaidi.
Aliyataja maeneo yanayokusudiwa kujengwa nyumba za kisasa na kulipa Jiji hadhi zaidi kuwa ni pamoja na Manzese, Mwananyamala, Mburahati, Kigogo Mbuyuni, Mkwajuni, Magomeni, Kinondoni Shamba na Mwenge, kwa upande wa Manispaa ya Kinondoni.
Kwa upande wa Manispaa ya Ilala, maeneo yaliyomo katika mpango wa NSSF ni Buguruni, Vingunguti, Mchikichini na Gongo la Mboto wakati kwa Manispaa ya Temeke ni Mbagala, Keko, Chang’ombe, Mtongani na Kichangani.
“Kwa sasa tupo katika maandalizi ya kujenga nyumba watakazoishi kwa muda watu watakaohamishwa kutoka eneo fulani ili kupisha ujenzi. Kila ujenzi utakapokamilika, wahusika ambao tutaingia nao mkataba watarudishwa katika maeneo yao na kuwa zamu ya watu wa eneo lingine la mradi. Tutakwenda awamu kwa awamu.
“Ni kazi ngumu, lakini tumeamua kushiriki kuijenga upya Dar kwa kuiondoa katika makazi holela,” alisema Kidula na kuongeza kuwa, jukumu wanalotarajia kulianzisha halitakuwa la kipindi kifupi.
Aliongeza kuwa, kufanikiwa kwa mradi huo kutasaidia kuboresha makazi, kuongeza idadi ya nyumba za kuishi zenye hadhi ya kimjini, kuboresha hali ya maisha ya wakazi wa maeneo husika, kutoa ajira na kadhalika.
Hatahivyo, ili kufanikisha hilo unahitajika ushirikiano mkubwa kutoka serikalini, katika halmashauri husika na wanajamii. Aidha, kwa upande wa NSSF, imeahidi kutoa elimu kwa umma kuweza kufahamu umuhimu wa miradi hiyo ya kuijenga upya Dar es Salaam.
Akizungumzia bandari ya nchikavu, alisema Shirika limeona haja ya kuwekeza katika eneo hilo kwani nchi inapoteza mapato mengi kutokana na bandari kuzidiwa uwezo na pia ufinyu wa mahali pa kuhifadhia makontena, hali inayosababisha mlundikano wa malori bandarini na barabara kadhaa za Jiji la Dar es Salaam zinazotumiwa na malori hayo.
Kwa sasa, uwezo wa bandari ya Dar es Salaam ni kupokea makontena 250,000 kwa mwaka, lakini kufikia mwaka 2009, idadi ya makontena kwa mwaka yalifikia 370,000.
“Utaona ni kwa jinsi gani bandari ilivyo na umuhimu mkubwa kwa uchumi wa nchi, lakini kwa sasa imeelemewa, kasi ya upakuaji mizigo ni ndogo na pia mizigo inayoshushwa haina pa kuhifadhiwa. Tutawekeza katika eneo hili kwa sababu ni biashara ya uhakika,” alisema na kuongeza kuwa, NSSF imeshapata eneo kubwa kwa ajili ya bandari kavu huko katika Kijiji cha Vihingo, Kisarawe, umbali wa kilometa 85 kutoka bandari ya Dar es Salaam.
Katika kuiongezea ufanisi bandari kavu, inakusudia kuanzisha mfumo wake wa kusafirisha makontena kwa njia ya reli, kwa NSSF kuwa na mabehewa yake, lakini kwa kiasi kikubwa ikitarajiwa kuzungumza na Tazara na Kampuni ya Reli nchini (TRL) iweze kutumia njia zake.