NYOTA WA FILAMU YA "THE MUSIC MAN" AFARIKI DUNIA...
https://roztoday.blogspot.com/2012/12/nyota-wa-filamu-ya-music-man-afariki.html
![]() |
| KUSHOTO: Suzzanne Douglas wakati wa uhai wake siku za hivi karibuni. KULIA: Akiigiza kama Susan Luckey. |
Susan Luckey - ambaye alijizolea umaarufu akiigiza kama binti wa Meya Shin, Zaneeta kwenye filamu kali ya "The Music Man" ya mwaka 1962 - amefariki dunia nyumbani kwake mjini Los Angeles akiwa na miaka 74 ... hii ni kwa mujibu wa binti yake, Shayna Reynolds.
Reynolds alieleza kwamba mama yake ambaye jina lake halisi ni Suzzane Douglas, hakuwa akisumbuliwa na maradhi yoyote kwa muda mrefu ... akafafanua kwamba kifo chake kimetokana na 'uzee.'
Imeelezwa Susan hakutaka mazishi ya kawaida yaliyozoeleka, badala yake mwili wake ulikaushwa na kuhifadhiwa kwenye 'sanduku lililopambwa' ambako wanafamilia wengine walizikwa.
Mbali na uhusika wake katika "The Music Man," Luckey alikuwa mwigizaji nyota sambamba na Shirley Jones mwaka 1956 kwenye filamu ya "Carousel" ... na alikuwa mmoja wa Wamarekani Wazawa katika filamu halisi ya "Peter Pan" iliyotengezwa na Broadway.