ABIRIA WACHANGISHWA PESA BAADA YA NDEGE YAO KUZIDI UZITO...
https://roztoday.blogspot.com/2013/01/abiria-wachangishwa-pesa-baada-ya-ndege.html
Uwanja wa ndege wa Liverpool John Lennon ambako ndege hiyo ilichelewa kwa zaidi ya Saa moja na nusu. |
Abiria katika ndege ya EasyJet iliyokuwa ikielekea Geneva walibebeshwa mzigo mzito wa zaidi ya bei ya sandwich ghali mara tu walipopanda ndege hiyo kwenye Uwanja wa John Lennon mjini Liverpool juzi.
Ndege hiyo iliyokuwa ianze safari Saa 4:05 asubuhi ilichelewa kwa Saa moja na nusu sababu ndege hiyo ilizidisha uzito kwa kilo 300. Mwishowe kapu la kukusanyia michango likaanza kupitishwa miongoni mwa abiria hadi zilipopatikana fedha za kutosha kuweza kuwalipa fidia abiria wanne watakaoshushwa.
Mhandisi Simon Lay - ambaye alikuwa kwenye ndege hiyo kwenda kuendelea na mapumziko ya kuteleza kwenye theruji - alisema rubani alipambana kupata abiria watakaojitolea kushuka sababu shirika hilo la ndege lilikuwa likitoa ofa ya Pauni za Uingereza 100 (karibu Shilingi 260,000 za Kitanzania) kama fidia.
Lay alisema kundi la abiria lililokete viti vya mbele kwenye ndege hiyo lilifanya fidia hiyo kuongezeka hadi kufikia Pauni 200 (karibu Shingi 520,000) kwa mtu mmoja kuwezesha abiria wanne kushuka katika ndege hiyo.
Alisema abiria waliobaki kisha wakaanza kuchangishana kusaidia kuwarejeshea gharama abiria 'waliotoboka mifuko' katika viti vya mbele.
EasyJet ilisema ndege hiyo ailikuwa imezidisha viwango vya uzito vilivyowekwa na mamlaka kufuatia kuwepo 'uwiano wa juu usio wa kawaida wa abiria wanaume'.
Kampuni hiyo ilisisitiza haikuwa sera yao kuruhusu kuchangishwa na kwamba 'lakini kama tunaweza kuanzisha hakuna utaratibu mwingine kati ya abiria uliofanywa'.
Abiria wanne walipelekwa Birmingham na kupandishwa kwenye ndege nyingine kuelekea Geneva majira ya 11:30 jioni.
Lay mwenye miaka 40, alisema: "Kuchangishana kunatokea wakati mwingine, niliweka Pauni mbili ambazo hazijavunjwa. Niliona watu wengine wakitupia noti za Dola tano.
"Inafedhehesha na kutahayarisha kwa EasyJet. Nilikuwa naenda safari ya kuteleza kwenye theruji na rafiki zangu na tulilipa zaidi kwa ajili ya ndege ya mapema hivyo kuweza kupata muda mrefu zaidi wa kucheza kwenye theruji.
"Walitangaza kwamba ndege imezidisha uzito kwa kilo 300 na rubani akaomba abiria wanaojitolea kushuka kwenye ndege.
"Kwanza walitoa ofa ya Pauni 100 za fidia na ndege ya Ijumaa lakini hakuna aliyeafiki hilo. Kisha wakabadili kuwa ndege ya siku hiyo kuanzia Birmingham. Kundi mbele ya ndege likachangishana na kufikisha Pauni 200 ili kuwashusha watu wanne.
"Abiria waliobaki kisha wakaweka Pauni chache kusaidia kuweza kuwashusha."
EasyJet ilisema katika taarifa yake: "EasyJet inathibitisha kwamba ndege EZY7279 kutoka Liverpool - Geneva ilizidisha viwango vilivyowekwa vya uzito kufuatia uwiano usio wa kawaida wa abiria wanaume na ubebaji mizigo kupita kawaida.
"Katika hali hii wa kujitolea wanatakiwa kushuka na EasyJet inatoa ofa ya Pauni 100 kama fidia na ndege mbadala. Abiria wanne waliojitolea walijitokeza mbele na ndege hiyo ikaruka muda mfupi baadaye.