DK MWAKYEMBE ASHITUKIA HUJUMA NZITO BANDARINI DAR...
https://roztoday.blogspot.com/2013/01/dk-mwakyembe-ashitukia-hujuma-nzito.html
Sehemu ya bandari ya Dar es Salaam. |
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ameshitukia hujuma nzito katika bandari ya Dar es Salaam, ikihusisha kuchomolewa kwa kipengele katika mkataba wa ujenzi wa boya la kupakulia mafuta kilichokuwa kinamtaka mzabuni kuacha vipuri vya zaidi ya dola za Marekani milioni tatu (Sh bilioni 4.8) mara baada ya kukamilika kwa mradi.
Hata hivyo, kukosekana kwa kipengele hicho sasa kutailazimu Serikali kuingia gharama hizo, badala ya kampuni ya Leighton Offshore iliyoshinda zabuni ya ujenzi wa boya hilo ambao kwa sasa umekamilika.
Kutokana na hujuma hiyo, Mwakyembe ameiagiza menejimenti ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Bodi yake kukaa kikao cha dharura leo ili kupata majibu ya nani alichomoa kipengele hicho kinachoibebesha mzigo serikali, na kwamba majibu ayakute mezani kwake ifikapo keshokutwa Jumatatu asubuhi.
Dk Mwakyembe alitoa agizo hilo baada ya kufanya ziara ya pamoja katika mamlaka hiyo akiwa na Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa, Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk Abdallah Kigoda na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, lengo likiwa ni kuangalia utendaji kazi.
Alisema kikao hicho cha dharura kinatakiwa kufanyika leo na baada ya majibu, atawasiliana na mawaziri wenzake na kuafikiana ni hatua gani za kuchukua, ikiwa ni pamoja na kumwajibisha mhusika.
“Tukishajua nani alihusika katika hili tutamwajibisha bila kigugumizi kwa kuwa hii ni hujuma, kikao kikikaa tutachukua uamuzi wa pamoja,” alisema.
Akizungumzia hilo, Simbachawene alisema anachofahamu ni kwamba mchakato wa kushindanisha zabuni ukishapita na mikataba ikasainiwa hakuna kurudi nyuma, hivyo kipengele kinapoondolewa wakati zabuni imeshashinda ni hujuma.
Kwa upande wake, Dk Mgimwa alisema kuwa kinachopaswa kuangaliwa kwanza ni kwanini hicho kipengele kiliondolewa na ni hatua gani zilizochukuliwa na mamlaka mpaka sasa.
Mbali na hayo, pia Dk Mgimwa aliiagiza mamlaka hiyo ifanye kikao cha pamoja na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) ili kuhakikisha wanaboresha mbinu za ukaguzi na kukuza mapato yatakayoboresha bandari nchini.
Naye Dk Kigoda alisema kuwa pamoja na uhaba wa fedha, lakini kuna changamoto kubwa ya uadilifu ambayo inapaswa kuangaliwa kwa undani na kutaka masuala ya kiuchumi yasijibiwe au kutatuliwa kisiasa.
Aidha Dk Kigoda aliliagiza Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kufanya kazi saa 24 kama ilivyo kwa taasisi nyingine ili kuendelea kuboresha huduma bandarini na kupunguza msongamano wa mizigo.
Pia aliiomba TPA kuwapatia eneo watakapoweza kujenga maabara ya mafuta ili kurahisisha kazi badala ya kwenda hadi Ubungo, jambo ambalo limekuwa likiwapotezea muda mwingi barabarani.
Katika hatua nyingine, Dk Mwakyembe aliagiza Mamlaka hiyo kusitisha leseni za kujenga Bandari kavu za magari na makontena katikati ya jiji na badala yake watoe leseni kwa wanaotaka kujenga bandari hizo nje ya jiji ili kupunguza msongamano.
“Iliamuliwa kwamba bandari kavu zijengwe ili kupunguza msongamano na kurahisisha kazi lakini bado nyingi zinajengwa hapa hapa katikati ya mji, hivyo naagiza kuanzia sasa hakuna kutoa leseni za ndani, toeni kwa wanaotaka kujenga nje mfano Kibaha na atakayetoa leseni kwa sasa za hapa ndani ya mji tutamuwajibisha,” alisema.
Aidha mawaziri hao walishangazwa na taarifa kwamba mamlaka hiyo haina mashine yenye ubora ya kukagua ‘kuscan’ mizigo iliyopo ndani ya makontena na iliyokuwepo ipo Bandari ya Tanga na haijafanya kazi kwa zaidi ya miaka miwili sasa.
Mapema Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Kipande Madeni alisema kuwa changamoto kubwa waliyonayo kwa sasa ni vitendea kazi na wameomba wasaidiwe ujenzi wa reli ili kuweza kusafirisha mizigo kutoka bandarini na kufikisha bandari kavu ili kuwarahisishia wateja wao usafirishaji na kupunguza msongamano bandarini.
Aidha alisema kuwa tatizo walilonalo kwa sasa katika bandari ni kina kifupi hivyo meli zinazotumika ni za kizazi cha pili na hivyo kukosa fursa ya meli zinazobeba mizigo mikubwa.