BABA ATAKA JINA LA BINTI YAKE ALIYEBAKWA NA WAHUNI LITAJWE...
https://roztoday.blogspot.com/2013/01/baba-ataka-jina-la-binti-yake.html
Baadhi ya wananchi wakiwasha mishumaa kuomboleza kifo cha binti huyo. |
Baba wa mwanafunzi wa India ambaye alibakwa na genge la wahuni hivi karibuni na kuibua kilio dunia nzima amesema alitaka jina la binti yake huyo kutangazwa hadharani hivyo kuwa kichocheo kwa waathirika wa vitendo vya ubakaji, wito ambao haraka ulinaswa na watumiaji wa mitandao ya kijamii na unaweza kushinikiza mamlaka kuruhusu utambulisho wake kuwekwa bayana.
Mwanafunzi huyo wa tiba ya viungo mwenye miaka 23 alifariki dunia Desemba 28 katika hospitali moja nchini Singapore, wiki mbili baada ya kubakwa na genge la wahuni ndani ya basi lililokuwa katika mwendo mjini New Delhi tukio lililoibua maandamano India nzima na nchi nyingine za jirani na serikali kuahidi adhabu kali zaidi.
"Tunataka dunia ifahamu nina lake halisi," baba wa msichana huyo alilieleza gazeti la Sunday People la Uingereza.
"Binti yangu hakufanya chochote kibaya, alifariki wakati akijilinda mwenyewe," aliongeza. "Najisikia fahari kwake. Kubainisha jina lake kutahamasisha wanawake wengine ambao wamekumbana na mashambulio kama hayo. Watapata ujasiri kutoka kwa binti yangu."
Mahojiano ya baba huyo yametema cheche kwa mapana na kuvutia mitandao ya kijamii. Jina lake lilikuwa mada kuu kwa watumiaji wa mtandao wa Twitter nchini India huku wengi, wakiwamo waandishi wa habari na waigizaji wa Bollywood, wakiafikiana na uamuzi wake wa kutaka kuwekwa hadharani jina la msichana huyo.
Mwelekeo wa vyombo vingi vya habari nchini India haukumtaja binti huyo, japo alikuwa akitambulishwa kama "Amanat", neno la kabila la Urdu likimaanisha "hazina", na baadhi ya chaneli za televisheni.
Msemaji wa polisi wa New Delhi alikataa kuchangia lolote pale alipoulizwa kama mamlaka zitachukua hatua dhidi ya mitandao ya kijamii au machapisho yatakayotaja jina la mwanafunzi huyo.
Kumekuwa na ongezeko kubwa la shinikizo nchini India kutaka kutajwa jina la mwathirika huyo wa ubakaji..
Mwanasiasa Shashi Tharoor wiki iliyopita alihoji uhalali wa kuendelea kuficha utambulisho wa binti huyo, na kushauri kuwepo sheria mpya za kuzuia ubakaji baada ya tukio lake, pendekezo la baba yake limeungwa mkono.
Sheria za India kwa jumla zinakataza utambulisho wa waathirika wa makosa ya ubakaji. Sheria zimelenga kulinda 'unyeti' wa waathirika na kuwaweka mbali na jicho la ukali la vyombo vya habari katika nchi ambapo makovu ya jamii yamehusishwa na ubakaji yanaweza kuharibu.
Baba huyi baadaye aliiambia Reuters kwamba hana pingamizi kwa vyombo vya habari kuanika jina la binti yake, lakini hakufafanua zaidi.