BABU LAIBUKA NA KUDAI BINTI ALIYEBAKWA NA WAHUNI KAJITAKIA...
https://roztoday.blogspot.com/2013/01/babu-laibuka-na-kudai-binti-aliyebakwa.html
KUSHOTO: Moja ya mabango ya wanaolaani ubakaji wakitaka wahusika wanyongwe hadharani. KULIA: Asaram Bapu. |
Aliyejitambulisha kama "mtu mashuhuri wa kiroho anayeheshimika' ametema cheche kuhusu uovu nchini India baada ya kusema kwamba msichana mwenye miaka 23 mwathirika wa ubakaji ambaye alifariki baada ya kushambuliwa na wanaume sita amechangia kwa kiasi katika shambulio hilo dhidi yake.
Asaram Bapu alisema kwamba binti huyo ambaye majina yake halisi ni Jyoti Singh Pandey, ambaye tukio lake limesisimua dunia nzima na kuchukuliwa kama janga la kitaifa nchini India, alikuwa 'na hatia kama ilivyo kwa wabakaji wake'.
Aliongeza kwamba angeweza kuwa karibu zaidi na wabakaji wake kama alitaka kulinda maisha yake binafsi.
Wanasiasa na watumiaji wa mitandao ya kijamii wamekemea vikali maoni hayo yaliyotolewa na mzee huyo wa miaka 71.
Mkanganyiko huo wa Asaram Bapu kuingilia kesi hiyo umekuja katika siku ambayo watuhumiwa watano wanaodaiwa kumbaka Jyoti wamefikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya mauaji, ubakaji na utekaji nyara.
Jaji aliamuru kwamba chumba cha mahakama kifungwe kwa wananchi baada ya zaidi ya watu 150 kujaribu kujisokomeza ndani ya chumba hicho chenye uwezo wa kuchukua takribani watu 30 wakati wa kuanza kusikiliza shauri la watuhumiwa.
"Watu watano hadi sita tu sio wahalifu," Asaram Bapu alisema. "Mwathirika ana hatia kama ilivyo kwa wabakaji wake.
"Alitakiwa kuwaita wahalifu hao kaka na kuwapigia magoti mbele yao kuacha."
Aliongeza: "Hii ingeweza kuokoa hatima yake na maisha. Mkono mmoja unaweza kupiga makofi? Sidhani."
Wanasiasa maarufu walikuwa wa kwanza kushutumu maoni hayo ya uchochezi, ambapo mwanasiasa mmoja wa upinzani aliyaita 'ya kujutia, kukera sana na kuumiza mno'.
Sandeep Dikshit, kutoka chama tawala cha Congress alisema, "Maoni kama hayo yanatakiwa kupingwa vikali kadri iwezekanavyo," wakati mwenzake Rashid Alvi aliongeza kwamba watu wa dini wanatakiwa 'kufikiri kwa kina' kabla ya kutoa maoni kuhusu mambo ya jamii.
Watu wengi wa India wametumia mitandao ya kijamii kuelezea kuchukizwa na mitazamo ya Asaram Bapu.
@SahilBulla akichangia kupitia mtandao wa Twitter: "Mpendwa Asaram Bapu, mkono mmoja hauwezi kupiga makofi lakini kidole kimoja kwa urahisi kinaweza kukuonesha tunachofikiria kuhusu wewe."
Mzee huyo pia alipinga vikali maandamano yanayofanywa na kundi la harakati za kijamii, ambao walikusanyika pamoja mjini Ahmedabad wakionesha mabango yanayosema "Asaram huna haya" na kuchoma sanamu zake.
"Tunataka kwamba Asaram aombe radhi kwa wanawake wa nchi hii na kumwomba afute maneno yake," alisema kiongozi wa maandamano hayo Sanjay Gadhvi huku akibainisha mipango ya kuchafua mabango aliyojitangaza Asaram na kuandamana kupinga maneno yake.
Msemaji wa mzee huyo alikanusha kwamba amekuwa hana utu kuhusu kifo cha Jyoti, lakini aliongeza: "Endapo binti huyo angetaja jina la Mungu au kumwita Mungu ndani yake angeweza kumshauri jinsi ya kuepuka makosa kama hayo."