BINTI WA MIAKA 12 ATISHIWA KUCHINJWA NA GENGE LA WAHUNI, ABAKWA...

Watuhumiwa hao wakiwa mahakamani katika picha ya kuchora.
Muathirika wa genge la ubakaji watoto alipelekwa kwenye msitu na kuambiwa kuwa angekatwa kichwa chake na watuhumiwa wake baada ya kukataa kufanya nao mapenzi, mahakama ilielezwa.
Msichana huyo alijaribu kudanganya kama amekubaliana nao kufanya kitendo hicho, lakini mmoja wa watuhumiwa hao, Akhtar Dogar akagundua kwamba alikuwa akiwadanganya.
Alipelekwa kwenye msitu ulio jirani, nje kidogo ya Oxford, ambako walimweleza: "Unafahamu tunachowafanya nguruwe, tunachinja shingo."
Msichana huyo kisha akalazimishwa kufanya mapenzi na kundi la wanaume kabla ya kutelekezwa kwenye msitu huo.
Noel Lucas QC akisoma mashitaka alieleza chumba cha mahakama kilichokuwa kimya: "Walimtisha, wakisema 'Unajua tunachowafanya nguruwe, tunachinja shingo zao'. Kama unavyotarajia, aliogopa sana.
"Gari nyingine iliwasili eneo hilo ikiwa na wanaume wengine wanne.
"Walimtishia kumkata kabisa kichwa chake."
Baada ya wanaume kuondoka na kumwacha hapo, alishindwa kujua njia ya kwenda nyumbani kwao na hivyo kulazimika kuwaita wanaume hao kwa ajili ya msaada. Walimchukua na kumpeleka kwenye nyumba ambapo aliwekwa kwenye chumba na wao kukaa kwenye chumba kingine huku wakicheka.
Mahakama ilielezwa muathirika huyo alikuwa na umri wa miaka 12 tu wakati alipoanza mchezo wa kutoroka na hivyo 'kuanza kuwindwa' na baadhi ya magenge ya wahuni.
Hatimaye akajikuta katawaliwa mno na washambulizi wake kiasi cha kusahau kwamba ilikuwa siku yake ya kutimiza miaka 15 ya kuzaliwa kwake wakati akiwa na wanaume hao.
Msichana huyo, ambaye sasa ana miaka 21, hakuwa na maisha ya furaha nyumbani kutokana na mama yake aliyekuwa na matatizo ya ulevi wa kupindukia.
Genge hilo la wanaume tisa linakabiliwa na tuhuma za kuwafanyia vitendo vya utu uzima na kuwashambulia vya kutisha wasichana wanaishi katika mazingira magumu wenye umri kuanzia miaka 11 - kuyafanya maisha yao kuwa ya mateso.
Wanaume hao, wote kutoka Oxford, wanadaiwa kuwapa pombe, cocaine na heroin wasichana sita kabla ya kuwabaka kwa kurudiarudia.
Kamar Jamil, 27, Akthtar Dogar, 32, Anjum Dogar, 30, Assad Hussain, 32, Mohammed Karrar, 38, Bassam Karrar, 26, Mohammed Hussain, 24, Zeeshan Ahmed, 27, na Bilal Ahmed, 26, wamekana mashitaka hayo dhidi yao. 
Mahakama ilielezwa msichana huyo alilalamika kwa polisi Septemba 2006 na kukabidhi taarifa iliyorekodiwa ambayo itasikilizwa mahakamani.
Ameshaishi kwenye nyumba kadhaa za kulelea watoto wa mitaani lakini alitoroka na wakati fulani aliwekwa kwenye makazi yanayolindwa.
Mahakama ilielezwa katika tukio moja alitoroka kutoka nyumba ya kulelea watoto wa mitaani siku ya Jumamosi akiwa na rafiki yake na kurejea akiwa kwenye teksi Jumatatu lakini wafanyakazi katika nyumba hiyo walikataa kumpokea.
Dereva teksi akamchukua na kumrejesha alikotoka na baadaye usiku huo alirejea kujiunga na genge hilo.
Watuhumiwa watatu kati yao walimnunulia zawadi kama uturi na kumpatia bangi na dawa za kulevya katika kile kilichoelezewa kama
'mambo ya kiutu uzima'.
Mwendesha mashitaka Noel Lucas QC alisema: "Mara ya kwanza walimfanya ajihisi wa kipekee kwa kumpa kipaumbele ambacho hakuwahi kupata nyumbani kwao.
"Wanaume hao, wakiwa wameshajua ni msichana wa mitaani, walikuwa walikuwa wakimlenga kwa ajili ya kukidhi haja zao za kufanya naye mapenzi."
Kundi hilo lilitaka kufanya naye mapenzi na kumweleza wangeteketeza moto nyumba yao na kumchoma moto kaka yake akiwa hai isipokuwa tu akikubaliana nao wanachotaka.
Alibakwa na genge hilo la wanaume katika Travelodge, nyumba ya kulala wageni na nyumba ambayo hakuna mtu yeyote anayeishi humo.
Lucas alisema: "Aliwaona wasichana wengine waliolewa dawa za kulevya katika majumba, wakati mwingine wakijilaza vitandani miguu juu wakiwa hawajitambui kabisa, wakingoja mzunguko mwingine wa pombe au dawa za kulevya."
Wanaume hao walijitambulisha kwake kama 'marafiki, kaka au mabinamu'.
Lucas alisema: "Wengi wao ni Waasia, waliobaki ni weusi."
Aliongeza: "Alikataa au kujaribu kukukuruka walimtandika vibao, kumvuta nywele zake na kumlazimisha kulala chini, hata kama alikuwa akilia.
"Ilifikia hatua akatulia na kuwaacha wafanye watakacho kwa hofu kwamba angepigwa."
Baadhi ya wanaume walipiga picha zake kwa kutumia simu zao za mikononi na kumwita majina kama 'msichana mchafu'.
Aliwaeleza polisi kuhusu 'uchizi' ambao kila mtu alikuwa akimhamasisha mwenzake.
Mapema jana mahakama hiyo ilielezwa jinsi Mohammed Karrar pamoja na watu wake kabla ya kufikishwa mahakamani, anadaiwa kutumia kifaa kwa muathirika mwingine alipokuwa na miaka 11 au 12 kumtoa mimba baada kuwa amepata ujauzito.
Wanatuhumiwa kwa kuwasababishia 'maumivu ya kimwili na kingono', mara kwa mara kuwapiga na kuwachoma wakati wakiwabaka waathirika wao.
Ushahidi wa simu kati ya watuhumiwa na waathirika utawasilishwa sambamba na ushahidi wa kipimo cha DNA.
Lucas alisema: "Ushahidi huo utaonesha kwamba wasichana hawa walikuwa wakilengwa makusudi kwa sababu walikuwa vijana wabichi."
Udhalilishaji huu unadaiwa kufanyika kwa zaidi ya kipindi cha miaka minane.
Kesi hiyo inaendelea.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item