MIAKA SABA YA KIFO CHA MAMA YETU, AGNES JACOB KASEGE...
https://roztoday.blogspot.com/2013/01/miaka-saba-ya-kifo-cha-mama-yetu-agnes.html
Ilianza sekunde, dakika, saa, siku, wiki, mwezi, mwaka na leo hii ni MIAKA SABA! Lakini ni kama jana kwa jinsi ulivyojaa mioyoni mwetu mama yetu kipenzi, AGNES JACOB KASEGE. Ni vigumu kukusahau mama hasa tukikumbuka tukio la Januari 16, 2006 majira ya Saa 4 usiku, ambapo ulinyamaza kimya na hukuamka tena mama yetu. Sisi tulikupenda mama lakini imani yetu inatuongoza kwamba Mungu alikupenda zaidi. Daima unakumbukwa sana na mume wako Mzee Eusebio Mwakitosi; watoto zako Regia, Aggrey, Zitta, Daudi, Patrick na Elijah; Wajukuu zako Agnes Sr., Enock, Beatrice, Isaac, Carine, Jacob, Eusebio, Colina, Agnes Jr., na Celine; Wakwe zako Baptista, John, Rose, Joyca na Immaculate Munde; bila kusahau ndugu, majirani na marafiki zako ambao uliishi nao kwa upendo na amani.
PUMZIKO LA MILELE UMPE EE..BWANA NA MWANGA WA MILELE UMWANGAZIE, APUMZIKE KWA AMANI MAMA, AMINA!