CHEKA TARATIBU...
https://roztoday.blogspot.com/2013/01/cheka-taratibu_11.html
Ilisikika kwenye kituo kimoja cha redio: "TAARIFA MBAYA TULIZOPATA MUDA MFUPI ULIOPITA KUTOKA NCHINI UTURUKI ZINASEMA ILE NDEGE ILIYOWABEBA WACHEZAJI WOTE WA TIMU YA SOKA YA YANGA PAMOJA NA VIONGOZI WATANO KUPIGA KAMBI NCHINI HUMO..." Unaambiwa kila mtu akaacha shughuli yake na kusogea karibu na redio kusikiliza kwa makini. Habari ikaendelea: "...IMETUA SALAMA UWANJA WA NDEGE BILA KUPOKELEWA NA WENYEJI WAO!" Duh, kila mtu akashusha pumzi...