WATOBOLEWA FIZI KWA SINDANO KUVUTIA WANAUME SENEGAL...
https://roztoday.blogspot.com/2013/01/watobolewa-fizi-kwa-sindano-kuvutia.html
Sahau kuhusu ung'arishaji meno au uzuri, wanawake nchini Senegal wamegundua uzuri wa tabasamu la kuvutia kwa viwango vya juu kabisa - kwa kuchora fizi zao kwa rangi nyeusi.
Wanawake katika nchi za Afrika Magharibi wanasema wazee wao wamekuwa wakifanya hivyo kwa miaka mingi na kudai pia kutoa tabasamu angavu, utaratibu ambao pia unalinda fizi na kukomesha harufu mbaya mdomoni.
Zoezi hilo halikufahamika sana kimataifa hadi hivi karibuni pale video iliponaswa ikionesha mwanamke anayeitwa Mariéme ambaye alikuwa akitobolewa kwa sindano.
Zaidi ya watu 17,000 wametazama Mariéme akipitia utaratibu huo wenye maumivu makali kwa njia ya mtandao.
Mariéme alisema amefikia 'kuvutiwa' na wazo la kuchora fizi zake rangi nyeusi ili kuweza kupata tabasamu maridhawa.
Anasema anamlipa mwanamke, ambaye ambaye anafanya kazi nje ya nyumba yao ya familia, karibu Shilingi za Kitanzania 2,000 kuweka rangi mchanganyiko wa mafuta yaliyochemshwa na siagi kwenye fizi zake.
Mchanganyiko huo kwanza unawekwa katika fizi kabla ya kuchomwa-chomwa kwa kutumia sindano mara kadhaa ndani yake.
Mariéme alisikia maumivu mwanzoni, anaonekana akimsukuma mpakaji rangi huku akibubujikwa machozi wakati maumivu yalipozidi kuwa makali.
Huku mchanganyiko wa rangi nyeusi ukiwa umezingira mdomo na uso wake, Mariéme alimudu kupata matabaka manne tu kati ya saba ambayo hapo kabla alikusudia kupakwa.
Alimweleza aliyekuwa akimhoji: "Inauma. Simshauri yeyote mateso haya."
Hatahivyo, licha ya maumivu baadaye anasema kuwa ana furaha kupita kiasi kwa jinsi anavyoonekana baada ya zoezi hilo.
Baada ya siku chache anasema: "Hakika inauma sana. Nilidhani nakufa lakini nilijaribu kujikaza kisabuni.
"Sijutii kwa sasa kufuatia kuwa na fizi zinazovutia mno. Ni muhimu kuwa mrembo na mwenye mvuto."
Mchoraji alisema zoezi hilo limekuwa likifanywa kwa miaka kadhaa nchini Senegal miongoni mwa wanawake na hata wanaume katika baadhi ya makabila wana fizi zilizopakwa rangi, ingawa anakiri wanawake wachache sana wamekuwa wakivutiwa katika siku za hivi karibuni.
Alisema: "Wanawake hawatakiwi kuwa na fizi nyekundu. Tabasamu lake lote linatakiwa kuwa la kupendeza. Tabasamu zuri linavutia wanaume."
Aliongeza: "Wanawake wachache mno wanafanya hivi lakini baadhi bado wanavutiwa hasa wanawake wanaotafuta wapenzi."