CHEKA TARATIBU...
https://roztoday.blogspot.com/2013/01/cheka-taratibu_14.html
Mwalimu kawaagiza wanafunzi kutengeneza televisheni kwa kutumia karatasi na kuziwasilisha darasani siku inayofuata. Kesho yake wanafunzi wote wakafanya kama walivyoagizwa isipokuwa mwanafunzi mmoja ambaye aliwasilisha karatasi tupu na mahojiano na mwalimu yakawa hivi. Mwalimu: Kwanini umeniletea karatasi ambayo hukuifanyia chochote? Mwanafunzi: Hapo imekamilika, hiyo ni FLAT SCREEN!