MTUHUMIWA ASEMA ALIPANGA KUMUUA BINTI BAADA YA KUMBAKA...

Eneo la Ravidas Camp ambalo wanaishi watuhumiwa wanne kati ya watano wa ubakaji.
Mtuhumiwa katika tukio baya la kubakwa msichana mwenye miaka 23 na kundi la wahuni ndani ya basi mjini Delhi amedaiwa kuwa aliwaeleza polisi kwamba alijaribu kumuua mwanafunzi huyo na rafiki yake wa kiume baada ya kumshambulia ili ashindwe kuwatambua.
Na katika jaribio ya kujaribu kuharibu ushahidi, Ram Singh aliripotiwa kuwaeleza polisi baadaye walisafisha basi hilo na kuchoma moto nguo za waathirika hao.
Singh alisema katika maelezo aliyotoa kwa polisi kwamba yeye na wenzake walijiandaa kula raha kwenye basi hilo mjini Delhi mwezi uliopita, wakikusudia kuteka nyara mwanamke, kumbaka na 'kufurahisha nafsi zao'.
Taarifa hiyo imesema Singh alianza kufikiria matukio hayo baada ya shambulio hilo, limeripoti gazeti la The Independent.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, taarifa inasomeka: "Nilisema kwamba endapo msichana huyo atapona, angeweza kututambua baadaye."
Taarifa hiyo kisha ikaendelea kufafanua jinsi alivyojaribu kumuua mwanamke huyo kijana.
Wanaume watano walioshitakiwa kwa ubakaji na mauaji walitarajiwa kufikishwa tena mahakamani jana.
Mtuhumiwa huyo, anasemekana kuwa na umri wa miaka 17, naye pia anashikiliwa na anatarajiwa kushitakiwa kivyake, wakati kesi ya watuhumiwa watu wazima ikisikilizwa kwenye mahakama maalumu.
Shambulio hilo lilimwacha msichana huyo akiwa amepigwa vibaya na kufariki wiki mbili baadaye katika hospitali moja nchini Singapore.
Katika mahojiano na gazeti la The Sunday Telegraph, mama wa msichana huyo ametaka wanaume hao waliomuua binti yake wanyongwe.
Alisema: "Roho yangu haitakuwa na amani kama wanaume hao waliomtesa binti yangu hawatanyongwa."
Mama huyo mwenye miaka 46 alielezea pia jinsi binti yake, mwanafunzi wa tibamaungo, akinong'ona, huku akikata roho kitandani, kwamba aliwataka 'wachomwe moto wakiwa hai'.
Wakili wa Singh, Ak Anand alisema juzi wanaume hao hawakuwa wakitarajiwa kutoa visingizio vyovyote watakapofikishwa mbele ya mahakama jana.

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item