JAJI WARIOBA AMWOKOA RAIS KIKWETE...
https://roztoday.blogspot.com/2013/01/jaji-warioba-amwokoa-rais-kikwete.html
Jaji Joseph Warioba. |
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amewaponda wanasiasa wanaodai kuwa Rais Jakaya Kikwete anaingilia madaraka ya Tume hiyo kwa kuzungumzia mchakato wa utoaji maoni na kusema, wanachokifanya ni siasa za upotoshaji.
Akizungumza na wanahabari Dar es Salaam jana, Jaji Warioba pamoja na kueleza kuhusu kuridhishwa kwa Tume yake na jinsi utoaji wa maoni binafsi ulivyokuwa, alisema kilichozungumzwa na Rais katika hotuba yake ya mwisho wa mwaka ni mchakato usio na kitu kipya kinachoweza kuwafanya wanasiasa wafikirie kuwa anaingilia kazi za Tume.
“Rais hapaswi kulaumiwa na wala wanasiasa hawapaswi kupotosha wananchi ili kutimiza malengo yao ya kisiasa. Alichokisema Rais si kitu kipya, kwa kuwa kimeelezwa katika Sheria ya Mabadiliko ya Katiba,” Jaji Warioba alisema na kuongeza:
Baadhi ya wanasiasa wanaitumia hotuba hiyo kupotosha wananchi ambao hata wao wanaruhusiwa kuuzungumzia mchakato huo wa Katiba kama alivyofanya Rais kwa sababu tayari umekwishazungumzwa katika sheria na wala hauna kitu kipya.
Alisema, “Sisi (Tume) hatuko hapa kufanya siasa na kutokana na maelezo ya Rais kwenye hotuba hiyo, hakuna uingiliaji wowote wa madaraka ya Tume aliofanya. Binafsi, nimekuwa nikiuzungumzia mchakato wa mabadiliko ya Katiba kila wakati, na ndiyo maana nasema hakuna jipya lililozungumzwa na Rais zaidi ya kuuelezea mchakato ambapo hata hivyo si kosa”.
Zaidi, Jaji huyo alihoji kuwa ingekuwa vipi endapo Rais asingezungumza lolote kuhusu suala kubwa kama hilo la mabadiliko ya Katiba ya nchi katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi na mwaka, wakati linagusa wananchi wote!
Maelezo yake yalitokana na madai ya wabunge wa Chadema; Tundu Lissu wa Singida Mashariki na John Mnyika wa Ubungo, kupitia vyombo vya habari kwamba Rais Kikwete anaingilia madaraka na kazi za Tume hiyo kutokana na kueleza mchakato wa ukusanyaji maoni katika hotuba yake ya salamu za Mwaka Mpya aliyoitoa Desemba.
Akihutubia hivi karibuni mkutano wa hadhara mjini Singida, Lissu aling’ang’ania kuwa Rais Kikwete amekiuka sheria na kutishia kufikisha bungeni hoja binafsi itakayomtaka Jaji Warioba afike bungeni kuelezea suala hilo.