RAFIKI WA PRINCESS DIANA ALIYELIPUKIWA BOMU ANGOLA ATOA LA ROHONI...
https://roztoday.blogspot.com/2013/01/rafiki-wa-princess-diana-aliyelipukiwa.html
KUSHOTO: Sandra (kulia) akiwa na mmoja wa wanawe. KULIA: Sandra akiongea na Princess Diana mwaka 1997. |
Alikuwa na umri wa miaka mitatu na alikuwa karibu kupata mguu wa bandia wakati Princess Diana alipomtembelea.
Picha za kutia uchungu za Sandra Tigica alipokutana na Binti Mfalme wa Wales mwaka 1997 ziliangaza kote duniani, zikionesha matatizo ya kutisha nchini Angola, ambako kulikuwa na idadi ya juu kabisa ya vifo duniani na ulemavu uliosababishwa na mabobu ya kutegwa ardhini.
Mguu wa Sandra ulikatwa katika mlipuko wa bomu miaka mitatu kabla wakati akikimbia mapigano katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini mwake.
Diana, ambaye alifariki mjini Paris katika ajali ya gari baadaye mwaka huo, alikuwa katika mji mkuu wa Angola, Luanda, kutangaza mchango wake kwa ajili ya kampeni ya Red Cross ya kukomesha matumizi ya mabomu ya kutegwa ardhini.
Sasa Sandra ameolewa na ni mama wa watoto watatu - na ndoto yake ni kwamba siku moja mke wa Prince William atabeba majukumu ya kazi nzuri iliyoachwa na mama yake.
Alisema: "Princess Diana alisaidia nchi yetu. Ni sehemu salama mno na shukrani nyingi ziende kwake. Ningependa kukutana na "Princess Kate". Nimesikia anafanya kazi nyingi za hisani na nafikiri lazima aendeleze kile alichoanzisha Princess Diana. Anatakiwa aje Angola." Sandra, ambaye alitazama harusi ya Kate na Prince William katika intaneti na kushitushwa na taarifa za ujauzito wake, aliongeza: "Nililia sana, kwa masaa mengi, siku Diana alipofariki.
"Alileta matumaini Angola. Kwa msaada wake wa kibinadamu kutoka nchi za nje, mabomu ya ardhini yanatoweka kidogo kidogo. Lakini tangu alipoondoka, watu wameshaanza kusahau."
Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni, ajali 89 zilizosababishwa na mabomu au milipuko ya mabaki ya vifaa vya kivita iliripotiwa nchini Angola mwaka 2011 - ambapo sita kati ya hizo zilihusisha watoto. Makadirio ya jumla ya ajali kwa zaidi ya miaka mitatu imeongezeka kutoka 23,000 hadi 80,000. Ilikuwa Januari 14, 1997, ndipo Sandra alipoongea na Diana huku wakiwa wameketi kwenye ukuta wenye vumbi katika Karakana ya Mifupa ya Bendinha iliyoko pembezoni mwa mji wa Luanda.
Sandra alikumbushia: "Alinipapasa uso wangu na kunieleza mambo mengi mazuri ikiwamo jinsi alivyopanga kuboresha hali katika nchi yangu."
Sandra amepata mguu bandia, lakini ameepukana na huu wa sasa - badala yake amechagua kutumia magongo. "Miguu inayotengenezwa hapa ni mizito mno na siwezi kutembea kawaida," alisema.
Anajipatia Pauni za Uingereza 130 kwa mwezi (zaidi ya Shilingi 338,000 za Kitanzania) kwa kuandika barua kwa ajili ya serikali za mitaa, wakati mumewe ni mwanajeshi. Wanaishi katika kibanda chenye ukubwa wa futi 20 kwa futi 40 kilichoezekwa kwa mabati kilichoko kwenye jimbo la Lunda Sul nchini Angola pamoja na watoto wao watatu wenye umri wa miaka minne, sita na minane, pamoja na mdogo wa kike wa Sandra mwenye miaka 13.
Ndani, picha ya Sandra na Diana wakijinafasi katika sehemu juu ya ukuta. Picha hii pia imekuwa ikitumika katika vitabu vya shule nchini Angola, na Sandra anafahamika kokote aendako kutokana na picha hiyo.
Anatazamia kuweza kuonekana katika filamu ijayo kuhusu miaka ya mwisho ya Diana, ikiongozwa na Naomi Watts.
"Siamini kama nitaonekana katika filamu kubwa - Niyakuwa nikicheza na mwigizaji wa kike!" Sandra alisema. "Sina televisheni hivyo sitaweza kuitazama. Lakini ningependa kwenda Uingereza na kuitazama."