KIJANA AMTANDIKA MWANAMKE BAADA YA KUITWA 'MNIGERIA ANAYENUKA'...

  
Hili ni tukio la kuogofya pale kijana mwenye gabhabu alipokuwa akijaribu kushikisha adabu mwanamke ndani ya treni ya chini ya ardhi baada ya kumfanyia vitendo vya kibaguzi.
Picha zilizopigwa kwa simu ya mkononi na kusambazwa kwenye mtandao wa YouTube juzi ziliwekewa kichwa cha habari "Mwanamke mbaguzi katika treni ya London apata anachostahili!"
Inaanzia kwa kifupi na malumbano baina yao - baada ya kijana huyo mwenye miaka 19 anayependa kuwa msanii kukanyaga kiatu cha mwanamke huyo.
Wawili hao walianza kutupishiana matusi, huku mvulana huyo akipiga kelele kwamba mwanamke huyo amemtamkia maneno ya kibaguzi, na kisha kumwita 'Mnigeria anayenuka'.
Malumbano yao yaliyoambatana na matusi yakafikia kwenye ugomvi, huku kijana akimrukia mwanamke baada ya kumtuhumu alikuwa amempiga kwa chupa.
Hatimaye, dereva wa treni hilo akaingilia kati na kuhoji kilichokuwa kikiendelea humo, na ndipo video hiyo ya dakika tatu ikafikia mwisho huku mapambano hao yakisitishwa

Post a Comment

emo-but-icon

Follow Us

Hot Reads

Recent

Comments

Side Ads

Traffic

Text Widget

Connect Us

item